Loading...
title : NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018
link : NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018
NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018
TIMU ya soka ya Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF), imeichapa bila huruma timu ya soka ya ZSSF 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka.
Mchezo huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa kuzikutanisha timu mbili za mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na ZSSF ambapo lengo la michizo hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya mashirika hayo mawili.
Mchezo huo uliianza kwa kasi kubwa iliwachukua dakika 4 NSSF kujipatia bao la kwanza baada ya mwamuzi wa mchezo huo Fikiri Yusuph kutoa Penalti baada ya beki wa ZSSF kuunawa mpira katika harakati za kuokoa, mshambuliaji wa NSSF Said Mwinyi aliipiga penalti hiyo na kuipatia timu yake bao la kwanza.
Kuingia kwa bao hilo la mapema kuliwafanya ZSSF kucharuka na katika dakika ya 10 nusura wajipatie bao la kusawazisha baada ya shuti kali lililopigwa na Juma Mbwana kugonga mwamba na kuokolewa na walinzi wa timu ya NSSF.
ZSSF waliendelea kulisakama lango la NSSF lakini walinzi wa timu ya NSSF wamkiongozwa na beki wa wa timu hiyo Hemed Kagobe waliweza kuondoa hatari hizo na kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa timu ya ZSSF.
Nahodha wa timu ya netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Pili Mogella, akipokea kombe la Ubingwa wa michuano ya tamasha la Pasaka kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete (kushoto), baada ya kuifunga ZSSF magoli 23-19 katika mchezo ulifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya soka ya NSSF, Mzee Mfaume, baada ya kuwafunga ZSSF mabao 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wachezaji wa timu ya soka ya NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa Kaimu Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa ZSSF, Abdallah Mbwana.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Hivyo makala NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018
yaani makala yote NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/nssf-mabingwa-tamasha-la-pasaka-2018.html
0 Response to "NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018"
Post a Comment