Loading...
title : RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO
link : RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO
RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii
BAADA ya ushindi mfululizo wa kikosi cha Ruvu Shooting na kuanza kujikita katika nafasi za juu, Msemaji wa klabu hiyo Masau Bwire ameweka wazi huo ni mwanzo tu kwani wamejipanga kuhakikisha wanawapapasa wale wote watakaokuja mbele yao.
Katika mchezo wa Ijumaa dhidi ya Azam,Ruvu Shooting iliweza kutoka na ushindi wa goli 2-0 na kwenye mchezo wa pili uliofanyika juzi wakiwa ugenini wakipambana na Ndanda waliibuka na ushindi wa goli 3-1.
Masau amesema mchezo wao dhidi ya Ndanda waliweza kufanya 'come back' na namna walivyorudi wakiwa nyuma kwa bao moja na kusawazisha kisha kushinda mchezo wa juzi.
Katika mchezo huo uliopigwa Nangwanda Sijaona, Ndanda ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kupata bao la mapema kabla ya Ruvu kuanza kusawazisha kisha kupata matokeo.Akizungumzia mchezo huo, Masau amesema kuwa waliweza kuupiga mpira mwingi wa kiulayaulaya huku akiitaja Yanga nayo ijiandae kupapaswa pale watakapokutana.
"Tumeupiga wa kiulaya, sisi mwendo wetu ni wa kupapasa tu, hakuna kumhurumia mtu maana tumezidi kuonyesha kuwa sisi ni bora. Tunawaomba na Yanga wajiandae maana tutakutana nao hivi karibuni" amesema.
Ruvu Shooting ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC na kuzidi kupambania tano bora katika msimamo wa ligi.Kwa sasa Ruvu Shooting wana alama 32 wakiwa katika nafasi ya saba wakipishana alama moja na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya sita na alama 33.
Hivyo makala RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO
yaani makala yote RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/ruvu-shooting-waahidi-kumpapasa-kila.html
0 Response to "RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO"
Post a Comment