Loading...
title : USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI
link : USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI
USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI
Assalaam Aleikum.
Salaam zangu za Mei Mosi
Kwanza sote tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma anaendelea kutupa uhai na uzima hadi siku ya leo.
Hakika pumzi hii ndio inatufanya tufurahi na kuhuzunika pamoja,pia ndio inayotufanya tuweze kuandika na kusoma maandiko mbalimbali ikiwemo andishi hili dogo
Jana pale uwanja wa taifa palifanyika mechi kubwa kabisa ktk ukanda huu wa Afrika Mashariki. Simba na Yanga zote za hapa jijini Dar.
Sio vyema kurejea kuwapa matokeo ila Alhamdulillah klabu yangu ya Simba imefanikiwa kushinda na kujisogeza karibu kabisa na ubingwa wa ligi kuu nchini
Nimeandika kujisogeza kwa kuwa bado hatujatwaa ubingwa.kwa sasa tunahitaji points tano tu ili tuweze kutawazwa ubingwa huu unaosubiriwa kwa hama na washabiki wote kote nchini
Kiukweli hzi points tunazohitaji tutazisaka kwa tahadhari zote na kwa kutambua kiu ya wanasimba.. tutaingia kwenye michezo ilobaki kwa nguvu kubwa na kwa umakini wa hali ya juu,sambamba na kuwaheshimu wapinzani wetu
Ukiachana na hayo nna vitu vwili very special nataka kuvisema hapa
Kwanza ni shukran kwa washabiki wetu..ktk maisha yangu yote nilioishi sijapata kuona washabiki kama wa Simba..
Ni watu wasikivu mno na wenye subira na upendo wa hali ya juu,ni watu wanaopenda futboll halaf ndio timu yao,wana ustaarabu uliopitiliza na wenye mapenzi yasio na shaka kwa klabu yao,
Kwenye ustaarabu huwa natolea mfano wa kitendo cha kutoa back pass kwa mchezaji Hassan kesi wakati akiichezea Simba kwa Donald Ngoma wa Yanga na kutufunga goli la kizembe zaid ktk historia ya derby hii
Inawezeka kabisa ilikuwa ni bahati mbaya,ila kilichostaajibisha muda mchache ujao mchezaji huyo alihamia Yanga tena kwa maneno mabaya ya dharau na kebehi..naapa Wallah kitendo kile ingekuwa kwa wenzetu kessi angeuhama mji huu na kurudi Morogoro (tamka Mrogoro)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI
yaani makala yote USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/ushindi-dhidi-ya-yanga-manara.html
0 Response to "USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI"
Post a Comment