Loading...
title : WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO.
link : WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO.
WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO.
Na John Nditi, Morogoro
POLISI Mkoani Morogoro inawashikilia wahamiaji haramu tisa ambao ni wa Ethiopia na Mtanzania mmoja ambaye ni dereva aliyekuwa anawasafirisha kwa gari lenye namba za usajili T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili T229 DBW ikitoka Dar es Salaam kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro , Ulrich Matei alisema kuwa tukio la kukamatwa kwa raia hao lilitoke Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi , mkoani Morogoro katika barabara ya Morogoro- Iringa.
Kamanda Matei alisema, raia hao walikuwa wamepakiwa wakiwa wamefichwa katika chasis ya gari hilo baada ya kutandazwa mbao ambalo lilikuwa likiendshwa na Mbaruku Kassim (40) mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam ikitkea kutokea Jijini humo kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Aliwataja raia hao wa Ethiopia waliokamatwa ni Taka Desta (24), Muluma Achiso (22), Mintensinot Workineh (23),Tesfhun Getachew (19), Muligeta Lalago (19), Zachewo Tikaso (20),Sekadu Abate (14), Asra Said (18) na Esafa Ercafo (22).
“ Raia hawa walihifadhiwa chini ya chisis ya gari baada ya kuwekwa mbao na wao kujificha eneo hili jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao , kitendo hiki ni kibaya “ alisema Matei.
Hata hivyo alisema , Polisi itaendelea kufanya ukaguzi na msako mkali katika maeneo ya njia zote kuu za mkoa huo ili kukomesha biashara hiyo haramu na watakaokamatwa wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kwa mujibu wa Kamanda wa mkoa kuwa, watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa ili waweze kukabidhiwa kwa Idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kuwafikisha mahakamani.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei akitoka kukagua gari iliyokamatwa na wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia, Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye gari lenye namba za usajili T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam wakitokea Jijini humo kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei akitoka kukagua gari iliyokamatwa na wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia, Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye gari lenye namba za usajili T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam wakitokea Jijini humo kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei akisoma majina ya wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia walikamatwa Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye gari lenye namba za usajili T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam likitokea Jijini humo kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia akiwemo na Mtanzania mmoja ambaye ni dwereva aliyetambuliwa kwa jina la Mbaruku Kassim (40) mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam ( wanne kutoka kushoto) wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kukamatwa Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye gari lenye namba za usajili T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili T229 DBW wakitokea Jijini humo kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.( Picha na John Nditi).
Hivyo makala WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO.
yaani makala yote WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/wahamiaji-haramu-tisa-raia-wa-ethiopia.html
0 Response to "WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO."
Post a Comment