Loading...
title : WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME
link : WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME
WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME
"Shemeji zangu walikuwa sita walinipiga sana kwa kweli kwa sababu ya kutaka kumiliki Mali za Mume wangu ambaye ni Marehemu" , ni mmoja ya wanawake wa Tarime akisimlia kwa masikitiko kutokana na ukatili alioupata baada ya kufiwa na mumewe, ambapo ndugu wa mume alilazimisha kumrithi yeye na mali za mumewe. Mila kama hizi zinazomkandamiza mwanamke zinapaswa kusitishwa.
"Tumekubali kabisa watoto wetu wa kike wasiendelee kukeketwa ,lakini bado jamii zetu hazituelewi tunaendelea kuwaelimisha ili nao wabadilike."- Mzee wa Kimila (Aliyesimama). Bado kuna kazi kubwa ya kumaliza swala la ukeketaji lakini kupitia elimu mbalimbali na mafunzo yanayotelewa kuhusu maswala ya ukeketaji juu ya hasara na madhara yake inaendelea kupunguza idadi ya wanaokeketwa.
"Kwa Tarime mwanamke kupigwa na kuvuliwa nguo hadhalani ilikuwa ni kitendo cha kawaida tu" - Sara Boniface (aliyesimama) , alielezea kwa kina kuhusu ukatili wa kupigwa ambapo aliongeza kwamba kwa sasa ukatili huo umepungua kutokana na elimu wanayoipata wanajamii juu ya ukatili wa kijinsia.
"Ukatili wa ukeketaji ulikuwa unafanyika hadharani kweupe, wazazi walikuwa wanalazimisha mabinti zao kukeketwa ili wapate mahali nyingi zaidi, ambapo fedha hizo ziwasaidie katika kupata kipato zaidi" - Nyakerandi Mariba. Swala hili limepungua sana kutokana na juhudi za wanamabadiliko kuendelea kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Hivyo makala WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME
yaani makala yote WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/wanamabadiliko-wasaidia-kupunguza.html
0 Response to "WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME"
Post a Comment