Loading...

Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu

Loading...
Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu
link : Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu

soma pia


Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa kila Mwananchi mwenye sifa za uchangiaji damu kuanzia umri wa Miaka 18 hadi 65 uzito wa Kilogram 50 ajitokeze kujitolea kuchangia damu ili kuiepusha Jamii kukumbwa na upungufu wa damu salama Nchini ambao wakati mwengine huleta athari.

Alisema upungufu mkubwa wa Damu uliojitokeza Mwaka uliopita hasa katika Kipindi Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa mujibu wa Taarifa za uchangiaji Damu Salama katika Maabara za Mahospitali Zanzibar ulipelekea kwenda kuomba Damu Tanzania Bara.

Akizungumza katika Bonaza la Uchangiaji Damu Salama lililoandaliwa na Mkoa wa Kusini Unguja na kufanyika Dunga Wilaya ya Kati Balozi Seif Ali Iddi alisema kwa mujibu wa Takwimu zilizopo inaonyesha kwamba mahitaji halisi ni chupa 1,250 kwa Mwezi kwa matumizi ya kawaida Unguja na Pemba.

Balozi Seif alisema shughuli za uchangiaji wa damu salama  humgusa kila mwana jamii  hivyo ipo faida kubwa inayopatikana licha ya kuokoa maisha ya walio wengi ambao hupatwa na matatizo ya kiafya lakini pia humrahisishia Mtu kuweza kupima maradhi mbali mbali bure bila ya gharama sambamba na kuelewa afya yake.

Aliwaasa Wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa maisha yao wenyewe wakiwa kama wana Jamii hasa wanapoelekea katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  ambao wengi hushindwa kuchangia Damu kwa wakati  pale wanapokuwa na mgonjwa anayehitaji huduma hiyo kwa haraka.
 Wataalamu wa Kitengo cha Huduma  za Damu Salama wakianza zoezi la kuwapima Wananchi waliojitokeza kuchangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja lililofanyika Wilaya ya Kati Dunga.
Wananchi mbali mbali wakipata ushauri nasaha kutoka kwa Wataalamu wa Kitengo cha Huduma  za Damu Salama kabla ya kuchangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja.
Afisa uhamasishaji wa kuchangia Damu kutoka Jumuiya ya Wachangiaji Damu Zanzibar Bwana Bakari Mabarawa aliyenyanyua  mikono akimpatia maelezo Balozi Seif jinsi ya Kampeni ya Uchangiaji Damu Salama unavyofanywa katika maeneo mbali mbali Nchini.
Mmoja wa Mchangiaji Damu aliyejitokeza kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Sabri Yussuf Ali akichangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja lililofanyika Wilaya ya Kati Dunga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wananchi wakati wa kichangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja lililofanyika Wilaya ya Kati Dunga.
Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu

yaani makala yote Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/balozi-seif-awataka-wananchi-kuchangia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu"

Post a Comment

Loading...