Loading...
title : BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB
link : BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB
BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB
*Mali, madeni, wafanyakazi kuhamishiwa TPB, wateja waombwa kuwa watulivu
Na Said Mwishehe, Globu
BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema Serikali ikiwa mmiliki mkubwa wa Twiga Bancorp imeamua kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa benki hiyo kwa kuiunganisha na benki TPB.
Akitangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam Naibu Gavana wa BoT Dk.Bernard Kibesse amesema kutokana na uamuzi huo wataja wa benki ya Twiga kuwa watulivu katika kipindi cha uunganishwaji wa benki hizo na kuendelea kupata huduma za kibenki kwa utaratibu utakaotolewa na menejimenti ya benki ya TBP.
Dk.Kibesse amesema muungano huo umeifanya BoT kusitisha usimamizi wa benki ya Twiga na masuala yote kuhusu benki ya Twiga Bancorp yatafanywa na benki ya TPB kuanzia kesho(Mei 17 ,2018)."Benki mpya ya TPB itakuwa na mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa kisheria chini ya kifungu cha 17 cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006,"amesema Dk.Kibesse.
Akifafanua kuhusu uamuzi wa kuunganisha benki hizo mbili, Dk.Kibesse amesema kwa mujibu wa Sheria ya mabenki na taasisi za fedha mwaka 2006, BoT imepewa mamlaka ya kusimamia shughuli zote za kibenki na taasisi za fedha nchini kwa lengo la kuhakiksha uimara na ustahimilivu wa sekta ya kibenki na fedha kwa ujumla.
"Ikumbwe BoT kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha sheria hiyo namba 56(1)(g)(i) namba 56(2)(a)-(d) Oktoba 28 mwaka 2016 iliiweka chini ya usimamizi wake benki ya Twiga Bancorp.
"Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na benki ya Twiga kuwa na upungufu mkubwa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Babenki na Taasisi za fedha mwaka 2006 na kanuni zake,"amesema.Amefafanua kwa wakati benki hiyo ilikuwa inahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kwake kutoa huduma za kibenki kulihatarisha usalama wa amana za wateja wake.
Hivyo katika kuboresha utendaji na ufasini wa benki zinazomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Serikali ikiwa mmiliki mkubwa wa Twiga Bancorp imeamua kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa benki hiyo kwa kuiunganisha na benki ya TPB.
Dk.Kibesse amefafanua kutokana na uamuzi huo mali, madeni na wafanyakazi wa benki ya Twiga wote watahamishiwa TPB huku akifafanua BoT itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uthabiti katika sekta ya fedha.
Ameongeza dhamira ni kuimarisha sekta ya mabenki na taasisi za fedha na mikakati ya Serikali ni kuimarisha mabenki kwa kuangalia namna ya kuzifanya kuwa na benki chache zenye tija.
Hivyo makala BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB
yaani makala yote BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/bot-yaamua-kuziunganisha-benki-za-twiga.html
0 Response to "BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB"
Post a Comment