Loading...
title : CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA
link : CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA
CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
CHAMA Cha Kijamii (CCK) kimekutana na wawakilishi kutoka mikoa 20 nchini kwa mara ya kwanza tangu kilipopata usajili wa kudumu mnamo mwaka 2012.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mkutano huo aliyekuwa mwenyekiti ambaye amejiuzulu nafasi yake Costastine Akitanda ameeleza kutokana na majukumu mengine aliyopewa ya kusimamia kilimo barani Afrika ameona aachie nafasi hiyo na anaamini Chama hicho kitafika mbali zaidi.
Akitanda ameeleza lengo la chama hicho ni kuwasaidia wananchi katika masuala mbalimbali ya kijamii hasa uchumi na kufafanua wanachama ndio wenye maamuzi katika chama katika kuhakikisha chama kinaenda mbele zaidi.
Kuhusu suala la ruzuku kwa vyama vya siasa Akitanda ameshauri kuwa ruzuku zitolewe kugharamia chaguzi ili kuwe na usawa katika uwakilishi na si kutolewa katika vyama.
Katibu wa chama hicho Renatus Muhabi ameeleza kuwa licha ya changamoto zilizopo kama vyama vingine kama vile kukosa ruzuku jambo linalosababisha ugumu katika kuendesha chama na amewaomba wanachama kuendeleza malengo ya chama hicho sambamba na kushika dola mwaka 2020.
Hivyo amewataka wasikatishwe tamaa na upotoshaji kuhusu hali ya kisiasa ya sasa kuhusu utendaji kazi wa awamu ya tano inayofanya mapinduzi katika jamii ya kitanzania.
Aidha amesema kuwa chama hiki kimepokelewa vizuri na wananchi hivyo wanataraji watafanya mapinduzi katika siasa na kuifikisha nchi katika mahali sahihi.
Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo ameshiriki mkutano huo na ameeleza kuwa amefurahi kualikwa na chama hicho ili aweze kutoa nasaha na ameeleza kuwa vyama vya siasa lazima viwe na urafiki kwa kuzungumza pamoja.
Amefafanua hiyo italeta siasa za amani na kusikilizana na hakuna chama pinzani bali vyote vina mlengo wa kuleta maendeleo nchini. Kuhusu ruzuku kwa vyama ameeleza ni muhimu zitolewe katika chaguzi ili kuweza kupata uwakilishi bungeni.
Mkutano huu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama ya siasa kama vile UPDP, SAUTI YA UMMA, TLP na Demokrasia Makini.
Hivyo makala CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA
yaani makala yote CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/cck-wajadili-hali-ya-siasa.html
0 Response to "CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA"
Post a Comment