Loading...
title : Mahusiano mazuri kati ya mwajiri na mfanyakazi kunaleta tija –Mwalwis
link : Mahusiano mazuri kati ya mwajiri na mfanyakazi kunaleta tija –Mwalwis
Mahusiano mazuri kati ya mwajiri na mfanyakazi kunaleta tija –Mwalwis
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi na waajiri ndio kunafanya kazi kufanyika na nchi kuweza kukua kiuchumi kutokana na uzalishaji unaofanyika.
Hayo aliyasema Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kazi, Andrew Mwalwis wakati kutoa zawadi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Lake Cement kilichopo Kimbiji jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kuendelea kwa kiwanda kunatokana na wafanyakazi kuwa na ari ya kufanya kazi.
Amesema kuwa kama kuna migogoro katika kiwanda hakuna uzalishaji ambao unaweza kupatikana na mwisho wa siku kiwanda kinafungwa.
Mwalwis amesema kuwa waajiri lazima wafuate sheria za nchi katika kulinda masilahi ya wafanyakazi na ndipo tunaweza kujenga uchumi wa viwanda pamoja na kusaidia watanzania katika suala la ajira.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Utawala wa Lake Cement, Giridhar Jadhao amesema kuwa wamejiwekea utaratibu wa kutoa zawadi kwa wafanyakazi kila siku ya wafanyakazi ili kuongeza tija na wengine kuweza kufanya vizuri.
Nae Afisa Rasilimali wa Kiwanda hicho, Julieth Domel amesema kuwa wafanyakazi wamekuwa na ari ya kufanya kazi na kufanya kiwanda kuendelea kuwepo.
Amesema kuwa ataendelea kuhakikisha wafanyakazi na wanaendelea kuwa na moyo wa kufanya kazi na kiwanda kuendelea kutoa huduma.
Mkurugenzi wa Idara ya Kazi Andrew Mwalwis akizungumza katika kiwanda cha Lake Cement wakati wa utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho, Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Utawala wa Lake Cement, Giridhar Jadhao akizungumza kuhusiana na wafanyakazi wa kiwanda hicho wanavyojitoa katika kufanyakazi ,Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Afisa Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Lake Cement, Julieth Domel akizunngumza kuhusiana na wafanyakazi kufuata sheria za kazi.
Mwenyekiti wa Tawi la Wafanyakazi wa Kiwanda hicho, Emmanuel Mayunga akizungumza kuhusiana na masilahi ya wafanyakazi katika kiwanda hicho na uchangiaji katika mifuko ya hifadhi ya Jamii.
Afisa Rasilimali wa Watu wa Lake Cement, Ahmed Mustafa akipokea zawadi kwa niaba ya mfanyakazi mwenzake katika utoaji zawadi kwa wafanyakazi wa kiwanda cha Lake Cement.
Afisa Usalama Mahala Pakazi katika Kiwanda cha Lakr Cement. Amina Likati akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa mwaka katika kiwanda hicho.
Sehemu ya wafanyakazi wakati utoaji wa kiwanda cha Lake Cement
Hivyo makala Mahusiano mazuri kati ya mwajiri na mfanyakazi kunaleta tija –Mwalwis
yaani makala yote Mahusiano mazuri kati ya mwajiri na mfanyakazi kunaleta tija –Mwalwis Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mahusiano mazuri kati ya mwajiri na mfanyakazi kunaleta tija –Mwalwis mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/mahusiano-mazuri-kati-ya-mwajiri-na.html
0 Response to "Mahusiano mazuri kati ya mwajiri na mfanyakazi kunaleta tija –Mwalwis"
Post a Comment