Loading...
title : DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO
link : DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO
DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO
MKUU wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga January Lugangika amewataka madiwani wa halmshauri ya Bumbuli kuhakikisha wanashiriki katika kukagua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuiepusha kujengwa chini ya kiwango na hivyo kukosa tija kwa wananchi.
Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la Kwehangara.
Alisema iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo inatoa mwanya kwa wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango vinavyotakiwa hali inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika. “Ndugu zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya maendeleo hili ndio jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo wakandarasi wanafanya miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake gharama inayotumika inakosa thamani yake”Alisema DC Lugangika.
Aidha pia alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Peter Nyalali kuweka utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi inayotekelezwa hususani miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa kutokana na wakandarasi”Alisema.Nay kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwasaidia kuwatatulia mambo mawili makubwa kwao kuyapatia ufumbuzi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali akizungumza katika kikao cha robo ya mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika eneo Jipya la Makao Makuu ya Halamshauri hiyo Kwehangala kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amiri Sheiza
Hivyo makala DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO
yaani makala yote DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/dc-lushoto-awataka-madiwani-kukagua.html
0 Response to "DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO"
Post a Comment