Loading...
title : MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA
link : MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA
MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
WAKULIMA wa zao la pamba wilayani Kakonko mkoani Kigoma wametakiwa kuwaepuka wanunuzi ambao hawatambuliki kisheria ili kuepukana na usumbufu wakati wa kuuza pamba zao huku Mkuu wa Mkoa huo akiwaagiza maofisa kilimo wote kuhamia vijijini kwa lengo la kutoa elimu kwa wakulima.
Kauli hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Kanyonza Wilaya ya Kakonko, na Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kigoma Joseph Lubuye wakati wa uzinduzi wa uuzwaji wa zao la pamba mkoani Kigoma.
Uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Kanyonza ambayo inaongoza kwa kilimo hicho katika Mkoa huo ambapo amewataka wakulima kuuza pamba yao katika kikundi cha ushirika na kampuni iliyopewa dhamana na Serikali ya kununua zao hilo.
Lubuye amesema kampuni itakayohusika na uuzaji na ununuzi wa pamba ni kampuni ya Kahama Cotton Campany Limited(KCCL) itakayoshirikiana na Chama cha Ushirika, lengo ikiwa ni kuhakikisha mkulima haibiwi na pamba inayouza na kununuliwa ni yenye ubora wa hali ya juu na kuepusha migogoro.
Amesema kwa mwaka huu pamba itauzwa kwa Sh.1,100 kwa kilo na kuwaomba wakulima kutumia nguo katika kubebea pamba na kusisitiza mkulima yeyote atakaeweka mchanga au maji kwenye pamba ili kuongeza uzito ataadhibiwa. Pia amewaomba wakulima kuwa wavumilivu kwani mwakani watapatiwa pembejeo za kilimo bure na viuwatilifu.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bregedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amewataka maofisa kilimo wote kuhamia vijijini kwa msimu huu wa uuzwaji wa pamba na msimu wote wa kilimo maofisa kilimo wote wanatakiwa kuondoka mjini na kuhamia vijijini kuwafundisha wakulima kulima mazao yenye ubora.
" Niwaagiza maofisa kilimo msimu wote huu wa uuzwaji wa pamba mje huku kukaa na wananchi, mtoe maelekezo watakacho kula wananchi na nyie mtakula hicho hicho kwani wananchi hawa ndio waajiri wetu.Mkoa wa Kigoma hatuhitaji matabaka ya watu ya wenye nacho na wasio nacho,"amesema na kuongeza
"Lazima tuhakikishe tunaunga mkono juhudi za wananchi kuweza kuinua uchumi wa wananchi na kipato kwa wakulima.
Sehemu ye shamba la pamba
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bregedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akizungmza mbele ya Wananchi wakati wa wakati wa uzinduzi wa uuzwaji wa zao la pamba mkoani Kigoma.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kanyonza Wilaya ya Kakonko wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa Uzinduzi huo.
Sehemu ye shamba la pamba
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bregedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akizungmza mbele ya Wananchi wakati wa wakati wa uzinduzi wa uuzwaji wa zao la pamba mkoani Kigoma.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kanyonza Wilaya ya Kakonko wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa Uzinduzi huo.
Hivyo makala MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA
yaani makala yote MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/maofisa-kilimo-wote-kigoma-watakiwa.html
0 Response to "MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA"
Post a Comment