Loading...
title : Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni.
link : Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni.
Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni.

Hayo yameelezwa jana na Mwanasheria wa mmiliki wa Kampuni ya PAP/IPTL, Harbinder Sing Sethi, Hajra Mungula, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mteja wake na kusema Sethi bado Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.
Wakili Mungula amesema kuwa watanzania kupuuza kwa taarifa zilizotolewa awali na watu wanaojiita kuwa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo.atika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wakili Hajra Mungula imesema kuwa yeye kama mwanasheria wa Sethi, amewasiliana na mteja wake, ambaye yuko rumande na kushangazwa na taarifa hizo.
Ilisema hivi karibuni kumeripotiwa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kampuni inayomilikiwa na Harbinder Sing Sethi imebadilisha uongozi katika ngazi za Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Mkurugenzi mtendaji wake.
"Taarifa iliyosambazwa na anayejiita mwenyekiti wa bodi mpya, Ambroce Brixio imemtaja yeye kuwa na cheo hicho na Joseph Makandege kuwa Mkurugenzi wake ambaye kwa miezi kadhaa sasa hajawahi kuonana nae ikiwemo hata kutofika mahakamani siku ambazo kesi imekuwa ikitajwa" imesema sehemeu ya taarifa hiyo.Wakili Hajra, aliandika katika taarifa hiyo kuwa taarifa hizo zimemfikia kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti halali na mmiliki wa kampuni hii ya kuzalisha umeme ya IPTL ambayo kimsingi inamilikiwa na kampuni anayoimiliki ya Pan Africa Power Solutions(PAP).
Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria huyo, pamoja na kuagiza wanasheria wake kuchukua hatua za haraka za kisheria mwenyekiti Sethi pia hana taarifa zozote juu ya mabadiliko hayo."Mwenyekiti Seth anapenda kuutaarifu umma kupitia sisi kwamba wazipuuze taarifa hizo kwa kuwa hazitokani na mamlaka halali za kisheria za kampuni hiyo," ilisema mwanasheria huyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni.
yaani makala yote Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/sethi-apinga-kuenguliwa-iptlakanusha.html
0 Response to "Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni."
Post a Comment