Loading...

MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Loading...
MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI
link : MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

soma pia


MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameutaka uongozi wa wilaya ya Gairo unamsimamia mkandarasi na kuhakikisha upanuzi wa kituo cha afya na unakwisha kwa wakati.

Akizungumza na uongozi na mkandarasi wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita ya kukagua maendeleo ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Kebwe amesema kuwa hajaridhishwa na kasi wanayokwenda nayo katika upanuzi wa kituo cha afya unaofanyika hivi sasa licha ya kuwa fedha za kituo hizo zote zimeshatolewa.

"Ni nini kinakwamisha ujenzi kuisha wakati fedha mmeshapewa???? amemuuliza Mkandarasi na Uongozi unaosimamia jengo hilo ... nawaomba sana, hebu fanyeni haraka maana kuna baadhi ya huduma wananchi wanakwenda kuzipatia mbali," amesema.

Amesema kuwa ipo haja ya kila mtu kutimiza majukumu yake bila ya kusukumwa sukumwa maana hali ya sasa ni kazi tu.

Awali akitoa maelezo ya ujenzi, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba amesema kuwa ujenzi huo umeshagharimu zaidi ya milioni 139 na baada ya kukamilika jumla ya wananchi wapatao 218,000 wataweza kupatiwa huduma huku vipimo vyote vikipatikana.


 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika tofali na mwiko) na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (aliyebeba tofali) kumsaidia fundi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikagua ujenzi kwa ajili ya kupanua eneo la kulaza, na sehemu ya kuhifadhia maiti wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya upanuzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

yaani makala yote MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/mkandarasi-wa-kituo-cha-afya-gairo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI"

Post a Comment

Loading...