Loading...
title : PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA
link : PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA
PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Usajili wa Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro umeendelea kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kusajili pamoja na changamoto kubwa ya mvua ambayo imeharibu miundombinu na kufanya baadhi ya maeneo kutofikika kwa kirahisi.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sanganjelu Kata ya Madege wilayani humo Afisa Usajili Wilaya ya Gairo Ndg. Godwill Mwamanga amewahimiza wananchi wanaoshiri zoezi hilo kuwa makini wanapojaza taarifa zao kwa kuhakikisha wanajaza taarifa sahihi naza kweli ili kuepukana na usumbufu hapo baadae.
‘Nawasihi sana muwe wakweli kwenye taarifa zinazohusu umri, makazi na uraia wenu ili taarifa zitakazo kusanywa zikajenge mfumo madhubuti wa Utambuzi wa Taifa wenye taarifa sahihi za watu” alisisitiza
Kwa sasa zoezi la Usajili linaendelea katika Kata ya Madege na Lesha ambapo Kata zingine za Msingisi, Rubeho, Chanjale, Iyogwe, Italagwe na Mkalama zimekamilisha zoezi. Kata za Nongwe, Gairo, Chagongwe, Chakwale, Kibedya, Idibo, Nongwe, Mandege, Chagongwe, Ukwamani, Magoweko na Ngiloli zitaendelea na zoezi kwa kuzingatia ratiba ya usajili iliyotangazwa na Mamlaka.
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa 21 inayoendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu lenye kulenga kuwapatia wananchi Vitambulisho vya Taifa.

Wananchi wa Kata ya Madege wakikatiza barabara kubwa ya Taragwe iliyojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha; kuelekea kwenye vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwenye Kijiji cha Sanganjelu wilani Gairo.
Wananchi wa kijiji cha Iyogwe wakisikiliza maelekezo ya utaratibu wa kusajiliwa kutoka kwa Msimamizi wa kituo ambaye hayupo pichani.
Ndg. Juma Ally mkazi wa Kata ya Iyogwe Wilaya ya Gairo – Morogoro akipigwa picha na kuchukuliwa alama zake za kibaiolojia wakati zoezi la Usajili likiendelea.
Wananchi wakazi wa kijiji cha Kilama wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakisikiliza kwa makini majina yao yakisomwa kuelekea kwenye chumba cha Usajili ikihusisha hatua ya kupigwa picha, kuweka alama za vidole na saini kileketroniki kwa kutumia mashine maalumu za kukusanya taarifa.
Afisa Usajili Wilaya ya Gairo Ndg. Godwill Mwamanga akizungumza na wananchi wakati wa kukagua maendeleo ya shughuli za Usajili kwenye kijiji cha Ngayaki kata ya Leshata.
Hivyo makala PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA
yaani makala yote PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/pamoja-na-mvua-kubwa-kunyesha-wananchi.html
0 Response to "PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA"
Post a Comment