Loading...
title : REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO
link : REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO
REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO
Aziz Rashid wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom wilayani Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom, Timu ya Rema 1000 FC imeifunga timu ya Airport Magoli 8-4 na kutinga fainali ambapo sasa itakutana na timu ya Dongobesh FC ambayo nayo imeshinda mchezo wake wa leo wa Nusu Fainali baada ya kuifunga timu ya Young Boys FC magoli 2-0 .
Mashindano hayo yanaandaliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na yanafanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom kwa udhamini mkubwa wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mkoani Iringa na Benki ya CRDB.
Mchezo wa Fainali utafanyika kesho kwenye uwanja wa huohuo kwa kuzikutanisha timu za Dongobesh FC na Rema 1000 FC ambapo pia kutakuwa na burudani mbalimbali za ngoma za asili wakiwemo pia wachekeshaji MC Pilipili na Katarina wa Karatu.
Aziz Rashid wa Rema 1000 FC ya Haydom Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya huku kiatu kikiwa kimechomoka mguuni wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom
Kocha wa timu ya Rema 1000 FC Bw. Jared Ochieng akiwaelekeza wachezaji wa timu yake kwa kuchora chini kutokana na makosa waliyokuwa wakisababisha katika mchezo huo wakati wa mapumziko.

Bw.Samson Madawabora ambaye ni Daktari katika Hospitali ya Haydom na mmiliki wa timu hiyo akiwapongeza wachezaji wake mara baada ya kutinga fainali ya michuano hiyo leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga pamoja na baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo wakifuatilia mchezo huo.
Hivyo makala REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO
yaani makala yote REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/rema-fc-yainyuka-airport-fc-magoli-8.html
0 Response to "REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO"
Post a Comment