Loading...

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW

Loading...
TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW
link : TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW

soma pia


TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW


Na.WAMJW

Serikali inatarajia kupata dola ya kimarekani milioni 512 kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI kutoka Serikali ya Marekani kupitia fungu la mradi wa dharura wa Rais wa kupambana na UKIMWI Duniani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa akipokea rasmi taarifa ya kutolewa fedha za UKIMWI kwenye hafla iliyofanyika kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa.

Dkt.Ndugulile alisema fedha hizo ambazo serikali itapatiwa zitatumika kwa ajili ya kununulia dawa za kufubaza makali ya Virus vya UKIMWI pia zitagawiwa kwa afua mbalimbali za kupambana na kuzuia maambukizi ya UKIMWI pamoja na uhamasishaji wa upimaji wa Virus vya UKIMWI nchini. 

Aidha ,alisema kiasi hicho cha fedha zinatakiwa kutumika ndani ya mwaka mmoja kwa kwa kujikita kwenye malengo ya Dunia ya tisini tatu(90,90,90) kwa kuhakikisha kwamba asilimia 90 ya watanzania wote wanaohisiwa kuwa na Virusi vya UKIMWi wanafikiwa,asilimia 90 ya wenye Virusi baada ya kupima wana pata tiba na asilimia 90 wanaopata tiba kuweza kufumbaza Virusi vya UKIMWI.

Alisema kama nchi imekuwa na changamoto kubwa sana na asilimia 90 ya kwanza ya upimaji kutokana na Takwimu za mwaka jana za hali ya maambukizi nchini zinaonyesha bado kuna changamoto kubwa hususan kwenye makundi ya vijana bado maambukizi yanaongezeka hasa kwa wasichana”vilevile kwa upande wa wanaume ambao ni wagumu kwenda kupima na wengine wanapima ila wanachelewa kuanza dawa na kutofuata misingi ya umezaji dawa na hivyo kufa zaidi”.

“Mkakati ambao tunautafakari na kuja nao ni ule wa mwananchi kuweza kujipima wenyewe kwa kutumia mate(Self-Test) hivyo kila mtu aweze kujijpima mwenyewe kwa kwenda kununua kipimo duka la dawa kama ilivyo kwa wanawake kujipima ujauzito”alisema Dkt.Ndugulile

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwatoa hofu wananchi kwamba Serikali haitawapima wanaume kwa nguvu kwenye ma bar bali itatumika utaratibu ule ule katika makundi yao kwa kuwapatia ushauri nasaha na kupima kwa hiari “hatusemi wanaume watapimwa kwa nguvu hapana utaratibu utakua ule ule hivyo wananchi msipate hofu” alisema dkt.Ndugulile

Alitaja mikakati mingine ni kwenda kuwafikia makundi mahususi ambayo inaonekana yana maambukizi makubwa ikiwemo ya wavuvi pamoja na migodini hivyo alitoa rai kwa watanzania kujitokeza ili kuweza kufikia asilimia 90 kutoka 52 ya upimaji wa Virus vya UKIMWI.Naye Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inm alisema nchi yake ipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kujenga Tanzania yenye afya nzuri.


Hivyo makala TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW

yaani makala yote TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/tanzania-kupata-dola-milioni-512-kwa_4.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW"

Post a Comment

Loading...