Loading...

UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?

Loading...
UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA? - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?
link : UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?

soma pia


UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?

Francis Daudi, Melukote Town!

Jana dunia ilisimama kupisha ndoa ya kifalme, Mwana Mfalme Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ mwenye miaka 33 alimuoa mwigizaji wa Marekani, Bi Meghan Markle mwenye miaka 36. Hii ndio kusema Meghan Markle ambaye alishaoana na Trevor Engelson kisha kutalikiwa mwaka 2013 anakuwa Duchess wa Sussex.

Wote wawili, yaani Prince Harry na Meghan Markle wanatoka katika familia za wazazi ambao wana historia ya kutalikiana! Lakini kikubwa zaidi ni kuwa haikutarajiwa Harry kuoa nje kabisa ya Ufalme wa Uingereza. Prince Harry kwa takribani miaka 7 iliyopita alikuwa akim‘DATE’ binti Chelsy Davy, mara kadhaa waligombana na kurudiana. Wakati Fulani mwaka 2011 ilitaarifiwa kuwa wameachana. Na sasa Prince Harry akaanza kuonekana Binti Cressida Bonas hadi mwaka 2014.

Kama utani vile, Prince Harry alimrudia Chelsy Davy ila wakati huu mwana mfalme alihakikisha taarifa hizi hazisambai tena mpaka lengo la ndoa litakapotimia. Maisha ya kujificha, huku wakisubiri kutangaza uchumba mwezi June, 2016 walivurugana tena.

Mwaka 2017 tetesi zikasambaa kuwa sasa mtoto wa Mfalme Prince Harry amekuwa na safari nyingi Marekani na huko kuna ‘Shemeji’ ambaye jina halikujulikana mpaka Harry alipoutobolea umma kuwa ana mchumba ambaye ni mwigizaji Meghan Markle. Ilikuwa habari mbaya na ya kushtua hasa kwa kuwa Meghan Markle anajulikana sana na kwenye jumba la ufalme ilionekana sasa wameingiliwa na ‘Mtalikiwa’.

Pamoja na mazonge hayo yote, Prince Harry aliwaalika Ma-Ex wake hapo jana! Wote walikuwepo Kanisani St. George’s Chapel. Mara kadhaa waandishi walijaribu kuwazunguka Chelsy Davy na Cressida Bonas. Haikuwezekana kwani ulinzi ulikuwa ni Mkali sana.
Kihistoria, Prince Charles ambaye ni baba wa Prince Harry aliwaalika Ex’s wake wakati wa Ndoa yake na Princess Diana iliyofanyika Julai 29, 1981. Kati ya hao ni Camilla, ambaye alikuja kuwa mke wa Prince Charles baada ya kutalikiana na Princess Diana mwaka 1985. Hii ndio kusema, Prince Charles alipata kuwa na Camilla kabla ya kumuoa Princess Diana. Ndoa ilipovunjika Prince Charles akamuoa Camilla ambaye ni mkewe mpaka leo. 
Inaelezwa kuwa historia inaweza kujirudia kwa Prince Harry na Chelsy Davy ambapo wamekuwa pamoja kwa muda mrefu Zaidi.



Hivyo makala UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?

yaani makala yote UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA? mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/ufalme-wa-uingereza-umeingiliwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?"

Post a Comment

Loading...