Loading...
title : WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
link : WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
SERIKALI mkoani Kigoma imewataka viongozi mbalimbali kuwa mfano katika zoezi la kuhamasisha wananchi kuleta watoto wao wenye umri chini ya miaka 14 kwenye chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.
Akizungumza jana Brigedia Jenerali Marko Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu , Emmanuel Maganga, wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kimkoa iliyofanyika wilayana hapa,alisema njia ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kupata chanjo, kutokufanya ngono katika umri mdogo, kubeba ujauzito katika umri mdogo pamoja na kuwa na wanaume zaidi moja.
"Njia ya pili ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini dalili za awali ili kupata matibabu mapema,"alisema .Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mlindoko alisema katika wilaya yake kuna jumla ya watoto 1325 wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14.
Alisema katika wilaya yake inatarajia kutoa chanjo kwa watoto 4974 na kwamba kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wametoa chanjo kwa watoto hao kwa asilimia 100.
Diwani wa kata ya Kazuramimba Nuru Kashakali, alisema amejitolea kuzunguka katika shule zote za msingi zilizopo kata yake ili kuwahamasisha watoto hao kujitokeza katika zoezi la kupatiwa chanjo.
Nao baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Uvinza Agustina Nzobanya mkazi wa Kazuramimba alisema yeye atahakikisha Watoto wake wote wanapatiwa Chanjo na kuendelea kuhimiza wananchi kuwaleta watoto wao ili kuepuka gharama zinazoweza kujitokezapindi wapatapo Ugonjwa huo.
Brigedia Jenerali Marko Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu , Emmanuel Maganga, akizindua chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi mapema jana wilayani humo.
Brigedia Jenerali Marko Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu , Emmanuel Maganga, akizungumza jambo mbele ya wananchi (hawapo pichani),mapema jana wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi
Hivyo makala WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
yaani makala yote WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/wananchi-wahamasishwa-kuwapeleka-watoto.html
0 Response to "WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI"
Post a Comment