Loading...
title : WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA KATIKA ELIMU WASISUBIRI HARUSI TU.
link : WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA KATIKA ELIMU WASISUBIRI HARUSI TU.
WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA KATIKA ELIMU WASISUBIRI HARUSI TU.
Na John Luhende
Mwambawahabari
Vijana wanaosoma shule za dini nchini wametakiwa kuwa mfano kwa jamii kwa kutenda na kuishi maisha ya uadilifu na maadili yanayo Mpendeza Mungu na Wana damu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Joseph Kakunda alipokuwa mgeni rasmi katika mahali ya shule ya Al-Farouq Islamic Seminary, huku akiwahimiza wawekezaji katika secta ya Elimu kuwekeza kwa wingi na kuahidi kuwa serikali itawaunga mkono.
Kakunda ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne 2018 kwa kushirikiana nafasi ya 4 kati ya shule 92 kiwilaya nafasi ya 27 kati ya shule 292, kitaifa 318 kati ya shule 3039.
Aidha amewataka Watanzani kuthamini elimu kuliko sherehe Arusi ambapo watu wengi wamekuwa wakichangia fedha nyingi na kuacha vijana wengi wakiwa hawana fedha za kuwagharamia katika masomo yao.
Amewataka wazazi kuwajali watoto wao na kutoa onyo kali kwa wazazi waliotelekeza watoto wao na kusema kuwa serikali itawashughulikia.
"Nampongeza Sana mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Makonda kwa kuanzisha kampeni ya kuwabaini walio waliotelekeza watoto Sisi s huku serikalini ametuzindua Sana na muimbaji endelee asitishwe na yeyote na mwezi wa sita tuta peleka sheria Bunge kuwa bana hawa watu " Amesema Kakunda.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Abass Yusuph amesema , pamoja na mafanikio hayo shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Mdahili Mdogo wa wanafunzi ambapo shule ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 34 kidato cha kwanza hadi cha nne lakini hadi sasa shule hiyo ina wanafunzi 136 tu, na mwitikio mdogo wa ulipaji ada .
Changamoto nyingine ni gharama kubwa ya utoaji mafunzo kwa walimu na kuomba serikali kuwasaidia katika utoaji wa mafunzo kwa kuwa lengo lao ni moja na serikali kutoa elimu kwa watoto wa Tanzania.
Hivyo makala WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA KATIKA ELIMU WASISUBIRI HARUSI TU.
yaani makala yote WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA KATIKA ELIMU WASISUBIRI HARUSI TU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA KATIKA ELIMU WASISUBIRI HARUSI TU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/watanzania-wahimizwa-kuchangia-katika.html
0 Response to "WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA KATIKA ELIMU WASISUBIRI HARUSI TU."
Post a Comment