Loading...
title : HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YA PANDISHA MADARAJA WATUMISHI 2200 NA BAADHI KUWAFUKUZA KAZI.
link : HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YA PANDISHA MADARAJA WATUMISHI 2200 NA BAADHI KUWAFUKUZA KAZI.
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YA PANDISHA MADARAJA WATUMISHI 2200 NA BAADHI KUWAFUKUZA KAZI.
MwambawahabariHALMSHAURI ya Manispaa ya Ilala, imewapandisha madaraja watumishi wake 2200 huku watumishi nane wakitimuliwa kazi kutokana na kukosa vigezo.
Watumishi 205 wenye elimu ya darasa la saba wanaendelea na ajira kwa mujibu wa taratibu za serikali. Akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, ambayo kiwilaya ilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, jana, Mkurugenzi wa halmshauri hiyo, Msongela Palela, alisema hatua hizo zimechukuliwa ndani ya wiki ya maadhimisho hayo.
“Wiki nzima iliyopita tulikuwa katika maadhimisho hayo na tuliona ni vema tukaaadhimisha kwa kujitathimini katika utendaji wetu kwa kuchukua hatua mbalimbali,”alisema Palela.
Aliongeza; “Tumewapandisha watumishi wetu madaraja kwa mujibu wa vigezo vyote na pia tulifanya uhakiki wa watumishi na kubaini watumishi nane hawa na sifa.Tumewaondoa,”
Wakati huohuo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, alisema halmshauri hiyo ilipokea malalamiko ya wananchi 2209 katika maadhimisho hayo.
Alisema malalamiko mengi yalihusu migogoro ya ardhi ambapo jumla ya malalamiko hayo ilikuwa ni 255.
“Katika wiki hii ya utumishi wa umma pia tulipokea malalamiko 501 yaliyohusu mikopo.
Watu wengi wanapata changamoto nyingi katika upataji mikopo hususan ile inayotolewa na taasisi za kifedha na serikali,”alisema Mpogolo.
Aliongeza; “Malalamiko kwa upande wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ilikuwa ni 200.
Asilimia kubwa ya vijana walilalamikia changamoto nyingi wanazo kumbana nazo katika kupata mikopo hiyo na tumekuwa tukiitatua kwa kushirikiana na mamlaka husika,”alisema
Mpogolo alisema, malalamiko menginwe yalihusu mirathi hususan watu kutapeliwa haki hasa watoto na wajane .
“Malalamiko 350 yalihusisha mikopo ya taasisi za kifedha .Wapo wananchi ambao walilalamika nyumba au mali zao kuuzwa baada ya kushindwa kurejesha mikopo waliyochukua katika taasisi hizo.Wengine waliingia mikataba bila kujiandaa namna ya kurejesha fedha,”alifafanua katibu tawala huyo.
Alisema, eneo lingine ambalo lililamikiwa ni upande wa ajira, ambapo wananchi walilalamika kufanya kazi katika mashirika, taasisi au kampuni bila mikataba na kufanya kazi katika mazingira magumu au kinyume na mikataba.
“Kwa kiasi kikubwa wafanyakazi wa kampuni binafsi za ulinzi na hoteli walijitokeza ambapo tumepokea malamiko 300,”alisema .
Alisema, malamiko mengineyo yalikuwa 285 na kwamba halmshauri itahakikishayanatafutiwa ufumbuzi wa haraka.
Hivyo makala HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YA PANDISHA MADARAJA WATUMISHI 2200 NA BAADHI KUWAFUKUZA KAZI.
yaani makala yote HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YA PANDISHA MADARAJA WATUMISHI 2200 NA BAADHI KUWAFUKUZA KAZI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YA PANDISHA MADARAJA WATUMISHI 2200 NA BAADHI KUWAFUKUZA KAZI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/halmashauri-ya-manispaa-ya-ilala-ya.html
0 Response to "HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YA PANDISHA MADARAJA WATUMISHI 2200 NA BAADHI KUWAFUKUZA KAZI."
Post a Comment