Loading...
title : RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA
link : RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA
RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA
Na Linda Shebby, Kibaha Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Everist Ndikilo amewataka uongozi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), kutokukaa maofisini na kusubiri wafanya biashara wawapelekee bidhaa zao wanazozizalisha kwani wanaweza kufanya udanganyifu hivyo kuweza kujipatia sifa ya ubora ambao hawakustahili.
Mheshimiwa Ndikilo amesema kuwa anategemea kuona bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Mkoa wa Pwani na nchi nzima kwa ujumla ziwe vinakidhi viwango vya ubora unaostahiki kwa kuzalisha bidhaa bora na zitakazoweza kuleta ushindani kwenye masoko yetu yote ya ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa ili kuitekeleza azma ya Uchumi wa Viwanda kwa ukamilifu ametoa rai kwa wenye viwanda na wazalishaji nchini kote kuzalisha bidhaa kwa kutumia vipimo stahiki ili kuweza kukidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa na kuweza kungia kwenye ushindani wa masoko ya Kimataifa.
Mheshimiwa Ndikilo amesema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) bado kunachangamoto nyingi kama vile umbali mrefu kutoka ofisi za Kanda hadi Mkoa na hivyo kusababisha baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kupata huduma kwa urahisi, huku upimaji huo umekuwa ukichukua muda mrefu hali inayosababisha kuendelea kuzalisha bidhaa zisizo na uthibitisho.
Hivyo amewataka TBS kufungua matawi ya ofisi zao kwenye Mikoa ikiwa ni katika kurahisisha huduma zao kwani zitasaidia kupunguza gharama kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuongeza ubora wa bidhaa.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amesema hayo wakati alipokua akifungua ,mafunzo ya vipimo ya siku moja yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani ambayo yameadhimishwa Mkoani Pwani leo.
Huku katika historia siku hii ya vVpimo Duniani huadhimishwa kila ifikapo Mei 20 kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kusainiwa kwa makubaliano ya kutumia vipimo vinavyofanana duniani kote ambayo yalifanywa kutoka mataifa 17 duniani, tarehe 20 Mei 1875.
Hivyo makala RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA
yaani makala yote RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/rc-pwani-awaagiza-tbs-kufanya-ziara-za.html
0 Response to "RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA"
Post a Comment