Loading...
title : KUMBILAMOTO ACHIMBAKISIMA SHULE YENYE WANAFUNZI 3000.
link : KUMBILAMOTO ACHIMBAKISIMA SHULE YENYE WANAFUNZI 3000.
KUMBILAMOTO ACHIMBAKISIMA SHULE YENYE WANAFUNZI 3000.
Mwambawahabari
Na John Luhende
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto leo amekabidhi kisima cha maji katika shule ya msingi Kombo ilyopo maeneo ya kata ya Vingunguti.
Akizungumza katika hafla hiyo kumbilamoto amesema, ameamua kuchimba kisima hicho katika shule ya msingi kombo kwa kuwa nimoja ya shule za sikunyingi lakini imekuwa na tatizo la maji kwamuda mrefu ambapo watoto na walimu walikuwa wanapata shida jambo ambalo lilikuwa lina hatarisha afya zao nayeye baada ya kutembelea na kujionea shida hiyo alistushwa na kutafuta namna ya kutatua tatizo hilo.
Amesema ,Kisima hicho kina uwezo wa kuhudumia wanafunzi wote wapatao 3000, na kuwa shukuru wafadhili walimsaidia kuchimba kisima hicho .
‘’Namshukuru sana Balozi wa Kuwait kwa msaada huo nilipo waeleza shidayangu kuwa nahitaji wani saidie kuchimba kisima katika shule hii hawakusita walinikubalia na sasa kisima kimekamilika kama unavyo ona hapa wanafunzi wanafurahia maji ‘’Alisema
Katika hatua nyingine Kumbilamoto ameanza kujenga ukuta katika shule hiyo baada ya kuombwa na walimu wa shule hiyo kwani ukuta ulipo unahatarisha maisha ya wanafunzi kuwa unatikisika hivyo umekosa uimara.
‘’ Ukuta huu nataka niujenge upya na sehemu zingine niuongee urefu ili wanafunzi wanaruka wasiweze nihatari kwa maisha yao nimeonyeshwa na mwalimu mkuu wanafunzi wanaruka hawaelewi lakuambiwa wanaweza kukutwa na majanga iwapo tutauacha hivi ,tayari haya matofari na mifuko hii nimekabidhi na ujenzai utaanza mara moja, ‘’ alisema .
Kwaupande wao Walimu na wanafunzi kataika shule ya msingi Kombo wamemshukuru Kumbilamoto kwa kuchimba kisima cha maji katika katika shule hiyo kwani wameteseka kwa muda mrefu hawakuweza kupa msaada .
‘’Namshukuru sana Mstahiki Meya kwa kutujali kwakweli hali haikuwa nzuri watato walikuwa wanapata shinda sana maji ya kunywa na maji ya chooni na hata bustanizetu hapa zilikauka lakini sasa mabo nimazuri kama unavyo ona zimekuwa za kijani tunaombatu sasa watuongezee matank Mungu amzidishie,’’ Alisema mwalimu mkuu Stella Mhando.
Naye mwakilkishi wa Afisa elimu wa manispaa ya iala katika hafla hiyo, Abdillahi Magoti Mchiya amesema, msaada huu umekuja wakati mwafaka na wanafunzi sasa watakuwa salama kwakuwa na maji ya kuaminika wataepukana ma magonjwa ya kuambukiza.
Picha za matukio mbalimbali katika uzinduzi wa kisima cha shule ya Kombo Vingunguti
Picha za matukio mbalimbali katika uzinduzi wa kisima cha shule ya Kombo Vingunguti
Hivyo makala KUMBILAMOTO ACHIMBAKISIMA SHULE YENYE WANAFUNZI 3000.
yaani makala yote KUMBILAMOTO ACHIMBAKISIMA SHULE YENYE WANAFUNZI 3000. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUMBILAMOTO ACHIMBAKISIMA SHULE YENYE WANAFUNZI 3000. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/kumbilamoto-achimbakisima-shule-yenye.html
0 Response to "KUMBILAMOTO ACHIMBAKISIMA SHULE YENYE WANAFUNZI 3000."
Post a Comment