Loading...
title : LHRC WAELEZEA CHANGAMOTO WALIZOPITIA MPAKA KUFIKA WALIPO SASA.
link : LHRC WAELEZEA CHANGAMOTO WALIZOPITIA MPAKA KUFIKA WALIPO SASA.
LHRC WAELEZEA CHANGAMOTO WALIZOPITIA MPAKA KUFIKA WALIPO SASA.
Na. Vicent Macha
Mwambawahabari
Mwambawahabari
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa katika kipindi cha utendaji wake amekutana na chagamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kukataliwa na wakazi wa Simanjiro alipoenda kuwapa elimu ya sheria.
Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Hellen Kijobisimba akiongea na waandishi wa habari Mapema leo jijini Dar es salaam, baada ya semina iliyowakutanisha wasaidizi wa kisheria kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam katika kongamano la wasaidizi wa kisheria Bisimba ambaye ameitumikia nafasi hiyo kwa miaka 22 alitaja matatizo mengine kuwa ni kunyimwa fedha na wahisani, uchache wa wafanyakazi ambapo walianza wakiwa wanane.
"Dhana yetu ilikuwa haieleweki kwa jamii, serikali na hata wanasheria lakini tuliweza kujenga hoja tukaeleweka na kufika hapa tulipo sasa" alisema Bisimba
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria ambapo baadaye walitoweka bila kufanyia kazi waliyofundishwa pamoja na kushindwa kuwafikia wananchi wote kwa wakati.
"Sintasahau siku tuliyoenda Terati, Simanjiro, Manyara kwa ajili ya kuwapa elimu kuhusu sheria na haki zao lakini wakatufukuza na kwenda kulalamika kwa wafadhili wetu kuwa tunawatumia wao ili tupate fedha na sio kuwasaidia" alisema Bisimba.
Alisema kutokana na uchache wa wafanyakazi walioanza nao walishindwa kufika maeneo yote hali iloyosababisha kutupiwa lawama na wananchi kwa kuwepo mjini pekee.
Aidha alisema baadhi ya wafadhili walikuwa wakinyima fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kwa sababu ya kukosa taarifa za matumizi ya fedha walizokwishawahi kuwapatia ambapo alisema walikuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na wasaidizi wa kisheria wa mikoani kushindwa kuwapa taarifa.
"Upatikanaji wa fedha ulikuwa mgumu baadhi ya wasaidizi wetu hawatoi taarifa ukipeleka maombi ya hela kwa mfadhili anaulizia kilichowahi kufanyika huko na kama hakuna fedha hazitoki hili lilikuwa tatizo kwetu na lilikwamisha miradi kwa baadhi ya Wilaya" alisema.
Hata hivyo Bisimba alisema anastaafu akiwa na fahari kwa kuanzisha mashina ikiwemo wasaidizi wa kisheria na waangalizi wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakiwasaidia wananchi kutambua haki zao pamoja na kuibua vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu bila woga.
Alisema kazi ya utetezi wa haki za binadamu si rahisi lakini lazima ifanyike bila woga kwa kusimamia sheria.
"Najivunia watu kuzifahamu haki zao na kusimama kuzitetea bila hata sisi kuwepo, kazi yetu si rahisi lakini lazima ifanyike bila woga, mda mwingine tunaambiwa sisi ni Chadema mara NCCR Mageuzi lakini maadamu tunajua sio tunaendelea kuchapa kazi" alisema Bisimba.
Mkurugenzi Mteule wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake Wakili Anna Henga ambaye ameteuliwa kuitumikia nafasi hiyo alisema ana kazi kubwa ya kuhakikisha haki za watu zinapatikana ambapo alisema amefanya kazi na Bisimba kwa zaidi ya miaka 10 hivyo ataendeleza mapambano pale yalipoishia.
"Anayeniachia kijiti amenilea kwa zaidi ya miaka 10, tutapambana kwa midahalo, makongamano na njia nyingine kuhakikisha haki zinapatikana, kipindi hiki tunaangalia zaidi sheria ya uhuru wa kujieleza na maudhui mtandaon" alisema Henga.
Wasaidizi wa kisheria kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini wakufuatilia semina.
Hivyo makala LHRC WAELEZEA CHANGAMOTO WALIZOPITIA MPAKA KUFIKA WALIPO SASA.
yaani makala yote LHRC WAELEZEA CHANGAMOTO WALIZOPITIA MPAKA KUFIKA WALIPO SASA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LHRC WAELEZEA CHANGAMOTO WALIZOPITIA MPAKA KUFIKA WALIPO SASA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/lhrc-waelezea-changamoto-walizopitia.html
0 Response to "LHRC WAELEZEA CHANGAMOTO WALIZOPITIA MPAKA KUFIKA WALIPO SASA."
Post a Comment