Loading...

Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu

Loading...
Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu
link : Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu

soma pia


Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu

 Na Daniel J. Mwambene, Afisa Habari Ileje
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Misitu (TFS) imeamua kuanzisha Shamba la Miti la Iyondo - Mswima ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2015/2020 ibara ya 31 vifungu vya b,c,d,e na f kuhusiana sekta ya Maliasili. 
Kwa mujibu wa Meneja wa Mradi wa Iyondo-Mswima Ndg. Deograsian Kavishe upandaji miti utaanza rasmi katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ikiwa baadhi ya kazi zilianza kutekelezwa na Mradi katika mwaka wa fedha 2017/2018. 
Kuanzishwa kwa shamba hili la Katengele kunaifanya Tanzania kuwa na mashamba ya miti ya kupandwa 23 yakiwa yanapatikana katika Kanda mbalimbali kati ya hayo manne yapo katika hatua ya uanzishwaji likiwemo hilo la Iyondo-Mswima wilayani Ileje. 
Kutokana na soko hili kuwa ndani ya msitu wa hifadhi na ili  kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kufuata Kanuni, Sheria na taratibu za uanzishwaji na uendeshaji wa miradi ya upandaji miti hapa nchini, soko hilo halistahili kuendelea kuwepo mahali lilipo, hivyo linatakiwa kuhamishiwa sehemu nyingine nje ya hifadhi zikiwemo kaya 13 zinazoishi ndani ya eneo hilo. Ujenzi wa miundombinu katika eneo lililochaguliwa utafanywa na serikali kupitia wakala wa Misitu (TFS). 
 Ili kuendeleza mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wa maendeleo TFS imeshirikisha Baraza la Madiwani, wataalam wa Halmashauri pamoja na Serikali Kuu. Michakato hiyo ilianzia kwenye vikao vya CMT, Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango pamoja na Baraza la Madiwani ambalo liliridhia kuhama kwa Mnada wa Soko hilo kutoka mahali lilipo na kwenda sehemu nyingine. 
 Baraza la Madiwani baada ya kujadili na kupitia mapendekezo ya vikao vilivyotangulia kisheria liliridhia juu ya kuhama kwa soko la Katengele kutoka mahali lilipo na kwenda Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala katika barabara ya Ibaba - Katengele ili kupisha uanzishwaji wa Mradi wa Shamba la Miti la Iyondo - Mswima. 
 Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya upigaji kura kufanyika ambapo Wah. Madiwani wane waliliridhia mnada wa Katengele uhamishiwe eneo la Ghala - Sange huku Madiwani 18 wakiridhia Mnada wa Katengele uhamishiwe Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndugu Haji Mnasi (aliyesimama) akizungumza kwenye Baraza Maalum kuhusu Mnada wa Katengele
Eneo la Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala panapotarajiwa kuhamishiwa Mnada wa Katengele.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje  Mhe.Ubatizo Songa akiongoza Wahe. Madiwani na Wataalam  wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walipotembelea eneo la Mradiwa Upandaji Miti la Iyondo-Mswima.Chini ni kitalu cha miti kilichopo Katengele-Ileje kikitarajiwa kubadilisha sura ya msitu wa Iyondo-Mswima wilayani Ileje.

Kusoma taarifa kamili BOFYA HAPA



Hivyo makala Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu

yaani makala yote Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/shamba-la-miti-la-iyondo-mswima.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu"

Post a Comment

Loading...