Loading...

Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea

Loading...
Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea
link : Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea

soma pia


Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja baina ya serikali na viongozi wa zamani wa Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) na kuamuru BMT kusimamia shughuli za mchezo huo wakati mchakato wa kuandaa uchaguzi mkuu ukiandaliwa. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Suzan Mlawi na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT. Alex Nkeyenge.

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipa mamlaka Baraza la Michezo la Tanzania (BMT) kusimamia shughuli za mchezo wa kuogelea wakati mchakato wa kuandaa uchaguzi mkuu wa chama hichon (TSA) ukiandaliwa.

Waziri Mwakyembe alisema hayo juzi katika kikao kilicho wakutanisha viongozi wa zamani walioenguliwa madarakani na wanachama wa chama hicho na Kamati ya Muda iliyomaliza muda wake wa miezi mitatu.

Alisema kuwa TSA  imekuwa na mvutano wa uongozi kwa muda sasa na kuhatarisha maendeleo ya mchezo huo ambao umeifanya Tanzania kutambulika zaidi kwa nchi za Kanda ya Tatu (Cana zone three) ikiwa ni mabingwa mara mbili mfululizo.
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkeyenge akizungumza.

Mwakyembe alisema kuwa mbali ya BMT kusimamia mchezo huo kwa sasa, viongozi wa zamani chini ya mwenyekiti Alex Moshi na Katibu Mkuu, Ramadhani Namkoveka wanatakiwa kuwasilisha ripoti ya utendaji wao ikiwa pamoja na taarifa za fedha (mapatona matumizi) kwa Msajili wa Klabu na Vyama Vya Michezo.

Alifafanua kuwa TSA ilitakiwa kufanya hivyo mwaka jana, lakini kutokana na hali ilivyokuwa, zoezi hilo lilisogezwa mbele mpaka Februari 28 mwaka huu, jambo ambalo halikufanyika.

“Nawaagiza kuwasilisha taarifa za utendaji wenu haraka iwezekanavyo kwa Msajili, kinyume hayo, sheria itachukua mkondo wake, serikali ya Awamu ya Tano  haina mchezo mchezo kwa viongozi ambao hawawajibiki na tutafanya haya kwa kila chama cha michezo,” alisema Mwakyembe.
Wanachama wa TSA wakifuatilia mkutano.

Alisema kuwa  hata viongozi ambao walijihudhuru nafasi zao, wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao mpaka pale walipoamua kuachana na uongozi.

“Naipongeza Kamati ya Muda kwa kukamilisha kazi zao kwa muda wa miezi mitatu kama walivyopewa na BMT na kwa sasa suala la Katiba litajadiliwa na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Msajili na viongozi wa zamani na Kamati hiyo siku ya Jumatano (June 13),” alisema.

Kamati ya Muda iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Imani Dominick na Katibu wake, Inviolata Itatiro iliyomaliza muda wake Juni 9 mwaka huu. Wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa, Alex Mwaipasi, Amina Mfaume na Anna Shanalingigwa.
Mwenyekiti wa zamani wa TSA, Alex Moshi akizungumza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda wa TSA, Imani Dominick akizungumza.


Hivyo makala Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea

yaani makala yote Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mwakyembe-aipa-mamlaka-bmt-kusimamia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea"

Post a Comment

Loading...