Loading...

MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl

Loading...
MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl
link : MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl

soma pia


MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
 Mwanafunzi wa Chuo cha Maabara Singida, Elia Mhina amekiri kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu dawa aina ya Paracetamol inayojulikana kama Panadol kwamba si salama kwa matumizi ya binadamu. 
 Hatua ya mwanafunzi huyo ambaye aliambatana na mzazi wake Mchungaji Emmanuel Mhina katika Ofisi za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), ilitokana na jitihada za mamlaka hiyo za kumtafuta hadi walipomkamata. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mhina alisema kuwa alipokea taarifa za uvumi kutoka kwende video iliyotumwa kwenye kundi moja la WhatsApp na kuifanya kuwa taarifa ya uhakika. 
 "Nilipokea video kweye kundi la Medical ambayo ilikuwa kwa lugha ya Kiingereza nami niliitafsiri kwa lugha ya Kiswahili na ndani ya siku tatu baada ya kuisambaza ilienea Tanzania nzima," Amesema Mhina. 
 Pia alieleza kuwa aliamini taarifa hizo bila ya kufuatilia kitendo ambacho kimesababisha hofu kwa watumiaji wa dawa hiyo. 
 "Niwaombe radhi Watanzania kwa ujumla, taasis na kampuni ya Paracetamol kwa makosa niliyofanya ambayo kimsingi sio mazuri hivyo naahidi hata nikipata ajira nitakuwa mwaminifu pia niwasihi vijana wenzangu watumie vyema mitandao tusisambaze taarifa bila kujua ukweli wake," alisema. 
 Baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Avest Kibaha, Emmanuel Mhina alisema alipewa taarifa kuwa mtoto wake amefanya makosa ya mtandao kwa kusambaza taarifa zisizo na ukweli na alikiri kufanya hivyo. 
 Alisema ni lazima watumiaji wa mitandao wawe makini na waangalifu kwani sio kila taarifa inatakiwa kusambazwa. 
 "Nawaomba vijana wajitawale na kuwa na mopaka katika kutumia mitandao ya kijamii kwani inaweza kubadili taswira ya kitu chochote. Pia wazazi tunapaswa kuwafuatilia watoto wetu ili kujua viashiria vyovyote vinavyoweza kusababisha taharuki kwa jamii," alieleza Mchungaji Mhina. 
 Kwa upande wake, Mwanasheria Mshauri wa TFDA, Iskari Fute alisema kitendo cha kusambaza uvumi ni kosa kisheria na kwamba likithibitishwa zipo adhabu mbalimbali ikiwemo kifungo jela au kulipa faini. 
 Fute alisema kwa mtu atakayebainika kutenda kosa hilo atatozwa faini ya kuanzia Sh laki moja hadi Sh milioni 10 au kifungo kisichopungua chini ya wiki mbili na kuendelea. 
 Tumeangalia kitendo na nia ya kufanya kitendo hiki tumeona kuwa hakuwa na nia ovu," alisema Fute. Pia aliwataka vijana kutumia somo hilo kuhakikisha wanatumia vyema mitandao ya kijamii na kwamba taarifa zozote zinathibitishwa na mamlaka husika.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agnes Kijo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu dawa aina ya Paracetamol inayojulikana kama Panadol kwamba si salama kwa matumizi ya binadamu uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Chuo cha Maabara Singida, Elia Mhina akizungumza na kuhusiana na kuhusika kusambaza taarifa za uongo za dawa aina ya Panado na kukiri kosa hilo kwa kuombaza msamaha kwa kile alicho kifanya katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mshauri wa TFDA, Iskari Fute akizungumza kuhusiana na sheria za kwa mtu anayesambaza taarifa za uongo katika masuala ya dawa na chakula Panado  katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. 


Hivyo makala MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl

yaani makala yote MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mwanafunzi-wa-chuo-cha-maabara-aomba.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWANAFUNZI WA CHUO CHA MAABARA AOMBA RADHI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO ZA DAWA YA PARACETAMOl"

Post a Comment

Loading...