Loading...
title : MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo
link : MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo
MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo
MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib (67) amezikwa jana jumapili kwenye makaburi ya Mwanakerenge mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Katika mazishi hayo yaliyowakusanya wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari familia ya marehemu iliwaomba waombolezaji waendeleze mshikamano aliouacha marehemu Taalib.
Kaimu Mwenyekiti wa SHIWATA, Deo Kway alisema wataendeleza juhudi za marehemu kuwaunganisha wasanii na wanamichezo kujikomboa kiuchumi.
Kway alisema wakati wa uhai wake marehemu Taalib aliwaunganisha wasanii mbalimbali na kuunda SHIWATA ambayo imefanikiwa kujenga kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga na kumiliki shamba la ekari 500 kwenye kijiji cha Ngarambe mkoa wa Pwani.
Marehemu Taalib alianza kuugua ugonjwa wa moyo kutoka mwaka jana na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha JK na baadaye kuruhusiwa na kuendelea kupata matibabu kila wiki.
Marehemu Taalib atakumbukwa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na juhudi zake za kuunganisha wasanii wa fani zote pamoja na kuwahimiza kuweka maslahi yao mbele ambapo alihamasisha ujenzi wa nyumba kwenye kijiji maalumu cha wasanii mkoa wa Pwani.
Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib jana jumapili kwenye makaburi ya Mwanakerenge mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib jana jumapili kwenye makaburi ya Mwanakerenge mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib katika mojawapo ya mikutano ta chama chake enzi za uhai wake.
Hivyo makala MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo
yaani makala yote MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mwenyekiti-wa-mtandao-wa-wasanii.html
0 Response to "MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo"
Post a Comment