Loading...
title : Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30
link : Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30
Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30
Na Greyson Mwase, Kagera
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuhakikisha linakamilisha kazi ya ukarabati wa miundombinu yote ya umeme nchi nzima kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Dkt. Kalemani ameyasema hayo leo tarehe 10 Juni, 2018 alipokuwa akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwenye ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) na ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji cha Rusumo kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 80 baada ya kukamilika Februari, 2020.
Alisema kuwa, kwa sasa nchi ina nishati ya umeme wa uhakika mbali na kuwepo kwa changamoto ya kukatika kwa umeme inayotokana na uchakavu wa miundombinu ya kusafirisha umeme.
“ Tulikubaliana na uongozi wa TANESCO kuhakikisha kazi ya ukarabati wa miundombinu ya umeme nchi nzima, inakamilika ndani ya miezi mitatu yaani hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu ili wananchi waanze kupata nishati ya umeme wa uhakika,” alisema Waziri Kalemani.
Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani alimtaka mkandarasi anayefanya kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika mkoa wa Kagera kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu, kampuni ya Nakuroi Investment Company Limited kuongeza kasi ya usambazaji katika mkoa wa Kagera ili mradi uweze kukamilika kwa wakati na wananchi kupata umeme wa uhakika.
Aidha, alizitaka taasisi za umma kama vile mashule, vituo vya afya na halmashauri kutenga fedha kwa ajili utandazaji wa nyaya za mifumo ya umeme (wiring) katika majengo yao ili waweze kuunganishiwa umeme mapema wakati wa utekelezaji wa mradi.
Wakati huohuo, Dkt. Kalemani aliitaka Serikali ya Mkoa na Wilaya kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda ili iwe rahisi kuwekewa miundombinu ya umeme wakati wa utekelezaji wa miradi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji umeme katika kijiji cha Kyerwa kilichopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali Mstaafu Shabani Lissu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akibonyeza kitufe kuashiria uwashaji umeme katika kijiji cha Kyerwa kilichopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kyerwa kilichopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na mkandarasi kutoka kampuni ya Nakuroi Investment Company Limited wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani)
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Katanda kilichopo wilayani Karagwe wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30
yaani makala yote Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/waziri-kalemani-aitaka-tanesco.html
0 Response to "Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30"
Post a Comment