Loading...

Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa

Loading...
Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa
link : Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa

soma pia


Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa

Na Mwandishi wetu,
WATAFITI waliokuwa wakifanyia utafiti mada kuhusu ukuaji bora wa miji nchini Tanzania, wamekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha katika mkutano mkubwa wa wadau chini ya mwavuli wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) siku ya Ijumaa tarehe 8 Juni 2018.
Katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida, ilielezwa kuwa Tanzania Urbanisation Laboratory (TULab)  ilikuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuonesha njia bora ya ukuaji wa miji nchini Tanzania kwa kuzingatia uchumi wa viwanda katika tafiti zake tatu.
TULab ilibuniwa mwaka jana kufuatia uchambuzi wa hoja ya Better Urban Growth in Tanzania ambayo ilijengwa katika kuhakikisha kunakuwepo na uelewa na kuuchochea mazungumzo ya kisera juu ya mabadiliko muhimu yanayotarajiwa katika kuelekea nchi yenye majiji makubwa yanayoshindana.
Mkutano wa mwishoni wa wiki uliitishwa kwa ajili ya kuona kilichojiri katika tafiti tatu kabla ya utafiti mwingine wa nne kufanyika, baadae mwaka huu.
Utafiti huo umelenga kutoa majibu kwa maswali yanayohusu maendeleo ya miji nchini Tanzania ambapo wadau wanatakiwa kuona.
Dkt.  Kida alishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kukubali kuwa mwenyekiti wa jukwaa hilo lenye umuhimu kwa maendeleo ya taifa.
Septemba mwaka jana kulianzishwa tafiti tatu ambazo zilichangiwa vyema na wajumbe na sasa mkutano huo ulikuwa unatoa taarifa za mwisho kuhusu nini wamekibaini katika tafiti hizo tatu.
Utafiti wa kwanza ulilenga kuelewa ugharimiaji wa miundombinu na huduma katika majiji makubwa 6 nchini Tanzania. Utafiti wa pili ulichunguza uhusiano kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na namna uhusiano huo unavyo athiri ugharamiaji wa miundombinu na utoaji wa huduma katika miji, na utafiti wa tatu ulilenga kuibua taarifa na takwimu ambazo zilikuwa hazijabainika hasa katika masuala ya maji.
pekee au watu binafsi pekee bali zinatakiwa kufanywa kwa ushirikiano.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa mabaara kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji yaliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dr. Idda Swai akiwsailisha utafiti juu ya uhusiano kati ya Serikali kuu na serikali za mitaa na athari zake katika kutoa huduma kwa wananchi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Mussa Martine akiwasilisha mada kuhusu huduma za tafiti za kifedha kwenye miji wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mtafiti Mshiriki kutoka Taasisi inayoshughulikia makazi ya watu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dr Nathalie Jean-Baptiste akiwasilisha mada kuhusu utafiti uliofanywa wa maisha ya kila siku ya wananchi kwenye miji ya Tanzania wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Bw. Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini, akielezea mipangilio ya programu hiyo kuelekea mabadiliko ya miji iliyopangwa wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete wakijadiliana jambo wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa

yaani makala yote Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mwongozo-wa-ukuaji-bora-wa-miji-wazidi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa"

Post a Comment

Loading...