Loading...
title : NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKA WANAO HUJUMU SHIRIKA LA RELI WACHUKULIWE HATUA
link : NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKA WANAO HUJUMU SHIRIKA LA RELI WACHUKULIWE HATUA
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKA WANAO HUJUMU SHIRIKA LA RELI WACHUKULIWE HATUA
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amewaagiza askari polisi kitengo cha reli kuwakamata watu wanaotuhumiwa kupiga mawe treni pindi zinapopita kwenye maeneo yao na kuhasababisha uharibifu ambao huigharimu serikali pesa nyingi katika matengenezo vingine watawajibishwa wao
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, alipotembelea Karakana ya Tazara iliyopo Jijini Mbeya.Amesema wapo baadhi ya watanzania wamekuwa wakiendelea na vitendo vya kuhujumu treni hivyo lazima wachukuliwe hatua kali ili kukomesha vitendo hivyo kwa kuhakikisha zinatolewa adhabu kali kwa watako bainika kufanya vitendo hivyo.
Waziri Nditiye amewataka madereva wa treni kusimamisha treni endapo itatokea kuna baadhiya watu wamefanya tukio la kupiga mawe treni mara iwapo safarini ili wahusika wakamatwe na kuhojiwa ili watoe sababu za kufanya kitendo hicho sanjali na kuchukuliwa hatua mara moja.
Wakati huo Naibu Waziri , amewahakikishia wafanyabiashara na wachuuzi kuwa hatua ya uimarishaji wa usafiri na usafirishaji kupitia Reli nchini,uko pazuri na tayari muda wa kuondoa mizigo mizito inayotumia malori umefika.Amesema katika kuimarisha usafiri huo, zaidi ya shilingi bilioni 10 zimetolewa na serikali kuboresha vichwa vya magari moshi na karakana mbalimbali nchini.
Amesema serikali haitegemei kuona malori ya kiendelea kusafirisha mizigo mizito ambapo wakati mwingine yamekuwa chanzo cha kuharibu miundombinu ya barabara pamoja na kuua soko la Tazara.“Barabara hizi zimejengwa kwa gharama kubwa sana, tunategemea mizigo hiyo kuanza kusafirishwa kwa kutumia njia ya reli na kwamba ni jukumu la wafanyakazi kuanza kuwashawishi wateja wao wa zamani na wapya ili wafanye kazi na Tazara,”amesema.
Hata hivyo amesema ,serikali haiwezi kuendelea kuwalipia mishahara lazima itafika pahala ambapo itasitisha na kuiacha Tazara iendelee na majuku yake kwa kujiendesha yenyewe, hivyo wanapaswa kujipanga kwa kuwa wabunifu.
Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kulia akisikiliza maelezo kutoka kwa Boniface Phiri ambaye ni Mhandisi uzalishaji kiwanda cha kuzalisha mataaluma ya Reli kwa kutumia zege kinachomilika na Tazara kilichopo katika Kijiji cha Mswiswi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kulia akipokea ufafanuzi kutoka kwa Boniface Phili Mhandisi uzalishaji kiwanda cha kuzalisha mataaluma ya Reli kwa kutumia zege kinachomilikiwa na Reli ya Tazara kilichopo katika Kijiji cha Mswiswi Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya

Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kulia akisikiliza maelezo namna ya utengenezaji wa mataaluma ya reli kwa kutumia zege kutoka Mhandisi Boniface Phili Mhandisi uzalishaji kiwanda cha kuzalisha mataaluma ya Reli kwa kutumia zege kinachomilikiwa na Tazara kilichopo katika Kijiji cha Mswiswi Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya
Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye pili kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa mafundi ya karakana ya Reli ya Tazara iliyopo katika kituo cha Iyunga Jijini Mbeya
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKA WANAO HUJUMU SHIRIKA LA RELI WACHUKULIWE HATUA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKA WANAO HUJUMU SHIRIKA LA RELI WACHUKULIWE HATUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKA WANAO HUJUMU SHIRIKA LA RELI WACHUKULIWE HATUA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/naibu-waziri-wa-uchukuzi-ataka-wanao.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKA WANAO HUJUMU SHIRIKA LA RELI WACHUKULIWE HATUA"
Post a Comment