Loading...

NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE

Loading...
NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE
link : NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE

soma pia


NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam limetoa mashine za kupima shinikizo la damu 12 zenye thamani ya Sh.5,000,000 kwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa lengo la kuboresha utoaji huduma hospitali hapo.

NSSF imesema vifaa tiba hivyo vitatumika kwa Watanzania wote watakaofika kupata tiba Hospitali ya Wilaya ya Temeke.Pia vitatumika kutoa huduma kwa wanachama wao wapatao 4000 ambao wanatibiwa hapo.

Akizungumza leo katika hosptali hiyo baada ya kukabidhi mashine hizo Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke Barnabas Ndunguru amesema wametoa msaada huo kutokana na maombi ya hospitali hiyo.

Pia amesema msaada huo ni moja ya jukumu la NSSF katika kurudisha fadhila kwa jamii ikiwa ni jitihada za kuisaidia Serikali katika juhudi za kuboresha sekta ya afya nchini.

Amefafanua NSSF Mkoa wa Temeke idadi ya wanachama wake wanaopatiwa huduma katika hospitali hiyo ni 4000 na kwa mwezi wanatoa fedha Sh.milioni 42 kwa ajili ya kulipia matibabu hayo."Hivyo tunaamini kutoa msaada huu wa BP Mobile Machine utasaidia katika kuwatibu wanachama wetu pamoja na wananchi wote ambao watakwenda kupata tiba,"amesisitiza.

Ameongeza msaada huo si mwisho na kuahidi kuendelea kusaidia kadri watakavyoweza kulingana na nafasi yao na kueleza wamekuwa wakisaidia jamii katika maeneo mbalimbali.Pia Ndunguru amesema NSSF wanalo fao la matibabu na kinachofurahisha zaidi wanachama wao wamekuwa wakipata huduma za afya za magonjwa yote isipokuwa TB na Ukimwi ambayo hayo huduma zake Serikali inatoa bure.

Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam Barnabas Ndunguru (wa pili kulia) akimkabidhi Ofisa Muuguzi wa Hosptali ya Temeke,Deodata Msoma vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi  milioni tano
Picha ya pamoja
Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam Barnabas Ndunguru (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi vifaatiba kwenye Hosptal ya Wilaya ya Temeke vyenye thamani ya shilingi Milioni tano .(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)



Hivyo makala NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE

yaani makala yote NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/nssf-yakabidhi-mashine-12-za-kupima.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE"

Post a Comment

Loading...