Loading...
title : Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko
link : Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko
Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Aidha kumekuwa mafanikio katika misako kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 20.06.2018 majira ya saa 22:30 Usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko maeneo ya Gerezani, Kata ya Ndandalo, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kukamata vipande tisa [09] vya meno ya Tembo na jino moja [01] la Kiboko vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa kilogram 30.
Thamani halisi ya meno hayo bado haijafahamika, jitihada za kuwasiliana na Idara ya Wanyama pori zinafanyika. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na msako mkali kuwatafuta watuhumiwa ambao walikimbia mara baada ya kuwaona askari. Aidha watuhumiwa wawili waliokimbia mmoja ametambulika kwa jina [Linahifadhiwa] Mkazi wa eneo la Magereza.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi MUSSA A. TAIBU anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi. Aidha Kamanda TAIBU anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na ujangiri na badala yake kujihusisha na shughuli halali pamoja na kulinda maliasili za nchi.
Imesainiwa na:
[MUSSA A. TAIBU - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko vilivyokamatwa Mbeya
Vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko vilivyokamatwa Mbeya
ACP MUSSA A. TAIBU -KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Hivyo makala Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko
yaani makala yote Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/polisi-mbeya-yakamata-vipande-tisa-vya.html
0 Response to "Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko"
Post a Comment