Loading...
title : RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO
link : RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO
RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amemuagiza mkuu wa Kituo Cha Polisi Gairo kuwakamata wale wote waliokula fedha za ujenzi wa maabara ya shule sekondari ya Idibo iliyiyopo katika Kata ya Idibo wilayani Gairo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara hizi karibuni Dkt. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema kuwa hawezi kuvumilia kuona shilingi Milioni 12 fedha za ujenzi wa maabara zilizotokana na nguvu ya wananchi zinaliwa na watu wachache tena bila kufanikisha malengo.
"Hivi kuna watu bado hawaelewi umuhimu wa kutunza fedha za umma??? Haiwezekani wananchi wajichange harafu nyie viongozi wa kijiji mle hela zao za maendeleo bila aibu, siwezi kuvumilia... Nakuagiza OCD Gairo na TAKUKURU kufanya msako watu hawa wapelekwe mbele ya sheria haijalishi walishastaafu au la!," amesema. Amesema kuwa ni vyema kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waendelee kuchangia maendeleo ya kijiji chao ila wanapotokea viongozi ambao si waaminifu ni vyema kuwaondoa haraka.
"Haiwezekani tokea mwaka 2014 maabara haijakamilika imeishia kujengwa msingi na kupandisha matofali kidogo huku fedha na nguvu za kujitolea wanachi ziwe zimepotea bure, naagiza viongozi waliokuwepo kipindi hicho wajisalimishe wenyewe huu ujinga hauwezi kuvumilika," amesema.
Aidha mbali na madudu hayo aliyoyakuta Dkt. Kebwe alitoa pongezi zake za pekee kwa uongozi wa wilaya ya Gairo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe kwa kuweza kusimamia vyema maendeleo ya wilaya na kuona inavyokuwa kwa haraka.
Amesema wilaya ya Gairo ilianzishwa mwaka 2013 lakini imeonyesha kuwa na miradi mingi ya maendeleo ambayo iko hai jambo linalompa faraja sana kwa kuona viongozi wanachapa kazi. "Wanawake wanaweza kweli, wilaya yenu inaongozwa na akina mama na wanachapa kazi vizuri sana, kwa hili lazima niliseme bila hata kificho... mpe mtu sifa zake akiwa hai maana hawa ndiyo wasaidizi wangu najua wanapitia changamoto nyingi ila wanazipangua na kusonga mbele,' amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba), Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi pamoja na pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya kijiji wakiwa katika ziara kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Hivyo makala RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO
yaani makala yote RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/rc-dkt-kebwe-ataka-waliokula-fedha-ya.html
0 Response to "RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO"
Post a Comment