Loading...

SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA

Loading...
SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA
link : SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA

soma pia


SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA

Image result for picha za joseph mbilinyi
Mwamba wa habari
Mwanamuziki Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ambaye ametoka jela hivi karibuni amelieleza Bunge leo Jumatano Juni 20, 2018 kwamba atatumia mawakili sita kulifungulia mashtaka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kupinga kufungiwa wimbo wake wa #219.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 bungeni leo Juni 20,  2018, Mbilinyi amesema kila taasisi imegeuka kuwa polisi ikiwemo Basata walioufungia wimbo huo uliovuja, kabla ya kuutoa rasmi.

Amebainisha kuwa Basata limetoa taarifa ya kuufungia wimbo huo wakati hawajui gharama alizotumia kuutengeneza.

“Wimbo umevuja wao  wanatoa statement (taarifa) ya kuufungia. Hawajawahi hata kuingia studio,  hawajui hata gharama. Wanataka wote tuimbe nyimbo za mapenzi,” amehoji.

Wakati akieleza hayo, Sugu alikatishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Juliana Shonza na kubainisha kuwa anachozungumza mbunge huyo wa Mbeya Mjini si sahihi.

“Wimbo unavuja vipi wakati uko kwenye mitandao. Hata mashairi yake ninayo hapa. Nyie wenyewe mlisema Basata wanafungia nyimbo bila taarifa,”amesema.

Amesema utaratibu unataka mtunzi kupeleka mashairi ya wimbo wake Basata kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuutoa katika redio, televisheni, mitandao ya kijamii na maeneo mengine.

Akijibu taarifa hiyo, Sugu amesema hawezi kumjibu naibu waziri huyo kwa sababu ni mdogo wake lakini anachofahamu ni kwamba yeye si  kama kama wanamuziki wengine  waliofungiwa nyimbo zao na baraza hilo.

“Sitampinga mheshimiwa Spika. Lakini  mimi sio kama Roma. Naiburuza mahakamani Basata  wimbo umevuja mimi sijautoa bado. Nina mawakili sita nitawaburuza mahakamani ndio watakoma,”amesema.

Taarifa ya Basata inasema imefikia hatua hiyo kwa kuwa una maneno ya uchochezi na kuhatarisha amani na utangamano miongoni mwa jamii.

Mbali na kuufungia Basata pia imetoa onyo kwa msanii huyo kuutangaza na kuusambaza kwa watu wengine.

Katika wimbo huo wenye beti tatu, mbunge huyo anazungumzia harakati zake za kisiasa zilizosababisha afungwe gerezani akiwa mfungwa namba 219.

“Muziki sikuuchagua, bali ulinichagua, nikafanya kweli na dunia ikanijua, nilichofanya kwa hili gemu mnakijua. Mbeya ndiyo inanitesa (wanaitaka Mbeya), najua Mbeya ndiyo inanitesa. Lakini bado napenda Mbeya inavyonitesa,” inasema sehemu ya kibao hicho.


Hivyo makala SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA

yaani makala yote SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/sugu-atishia-kuishitaki-mahakamani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SUGU ATISHIA KUISHITAKI MAHAKAMANI BASATA"

Post a Comment

Loading...