Loading...
title : RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
link : RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Dkt. Shein amefanya uteuzi huo kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu 119 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 .
Aidha amewateua wajumbe sita wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambao ni Bwana Mabrouk Jabu Makame, Bwana Feteh Saad Mgeni, Bwana Makame Juma Pandu, Dkt. Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdalla na Bibi Jokha Khamis Makame.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo umeanza leo tarehe 20 Juni 2018.
Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi walioteuliwa wataapishwa siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2018 saa 4.00 asubuhi Ikulu Mjini Zanzibar.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Hivyo makala RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
yaani makala yote RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/rais-dkt-shein-afanya-uteuzi-wa.html
0 Response to "RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR"
Post a Comment