Loading...
title : TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC
link : TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC
TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC
Na Hamza Temba-Arusha
Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) imezua mjadala mzito na mabishano makali katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Arusha juzi.
Mvutano huo ulisababishwa na hoja iliyowasilishwa na Tanzania ambayo ilitaka kuboreshwa kwa kifungu cha nne cha itifaki hiyo ambacho kinazitaka nchi wanachama kutangaza eneo lote la jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama kituo kimoja cha safari za utalii duniani.Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ilipinga vikali na hatimaye ikagoma kusaini itifaki hiyo ambayo imejadiliwa kwa zaidi ya miaka saba mpaka pale mapendekezo yake yalipoingizwa kwenye kifungu hicho.
Kifungu hicho kilikuwa kinasema, "Every Partner State shall market and promote the Community as a single tourist destination", (Kila nchi mwanachama itatangaza jumuiya kama kituo kimoja cha safari za utalii (duniani)).Tanzania ikapendekeza kwenye kifungu hicho uongezwe mstari unaosema, "while maintaining country identites" (huku kila nchi mwanachama ikibaki na utambulisho wake halisi).
Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasilisha mapendekezo ya Tanzania kwenye kifungu cha nne cha Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki.
Baadhi ya wajumbe wa Tanzania walioshiriki mkutano huo.
Hivyo makala TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC
yaani makala yote TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/tanzania-yaweka-msimamo-mkali-kwenye.html
0 Response to "TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC"
Post a Comment