Loading...
title : TOC FC MABINGWA WAPYA LIGI YA AWESO CUP 2018 PANGANI
link : TOC FC MABINGWA WAPYA LIGI YA AWESO CUP 2018 PANGANI
TOC FC MABINGWA WAPYA LIGI YA AWESO CUP 2018 PANGANI
TIMU ya TOC FC juzi walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Ushirika FC mabao 4-3 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye viwanja vya Kumba wilayani Pangani.
TOC ambao ni mabingwa walikabidhiwa kombe la Ubingwa,Medali na kitita cha sh.milioni 1 kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo (CCM).
Huku mshindi wa pili timu ya Ushirika FC walikabidhiwa kitita cha laki sita na medali wakati mshindi wa tatu akipata laki nne na medali kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kushindwa kutambiana ndani ya dakika tisini na hivyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ndipo TOC walipofanikiwa kuibuka videdea.
Hivyo makala TOC FC MABINGWA WAPYA LIGI YA AWESO CUP 2018 PANGANI
yaani makala yote TOC FC MABINGWA WAPYA LIGI YA AWESO CUP 2018 PANGANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TOC FC MABINGWA WAPYA LIGI YA AWESO CUP 2018 PANGANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/toc-fc-mabingwa-wapya-ligi-ya-aweso-cup.html
0 Response to "TOC FC MABINGWA WAPYA LIGI YA AWESO CUP 2018 PANGANI"
Post a Comment