Loading...
title : TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI
link : TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI
TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetoa Mafunzo maalum kwa wahandisi watakaosimamia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye skimu kumi na sita(16) zitakazojengwa mwaka ujao wa fedha, 2018/2019 kutoka kwenye kanda nane (8) za Tume ya Taifa ya umwagiliaji, Halmashauri za wilaya pamoja na wakandarasi, ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo uelewa na uzoefu zaidi wahandisi hao katika usimamizi wa mikataba na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.
Akizungumza katika warsha hiyo ya mafunzo ya siku tatu iliyofanyika Mkoani Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi wa uendelezaji wa miundombinu ya Umwagiliaji kutoka Tume hiyo Mhandisi, Pascal Shayo, alisema kuwa Tume imetoa Mwongozo wa ujenzi wa skimu za umwagiliaji na alisisitiza ya kuwa, wahandisi waliopewa mafunzo hayo wanatakiwa wasimamie ujenzi wa skimu hizo kwa kufuata mafunzo waliyoyapata ili kuhakikisha miundombinu hiyo inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa.
“Mhandisi atakayeshindwa kusimamia vizuri atachukuliwa hatua kwani kwa kupitia mafunzo haya wameshapata uelewa wa kutosha.”Alisisitiza
Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Sanifu na Uratibu wa Sekta Binafsi kutoka katika Tume hiyo Mhandisi Muyenjwa Maugo alisema warsha hiyo ina lengo la kuhakikisha miradi yote ya umwagiliaji inajengwa katika kiwango elekezi na wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa katika kilimo cha umwagiliaji na kuzalisha mazao bora.
“Lengo kubwa ni kujenga uwezo kwa wahandisi na wataalam wa umwagiliji ili kuweza kusimamia miradi ya umwagiliaji kwa ufanisi, na kupitia miradi hii tunaweza kuwafundisha wahandisi namna ya kutumia mwongozo uliyopo katika kusimamia shughuli za umwagiliaji.” Alibainisha Maugo.
Awali imeelezwa kuwa ,ujenzi wa skimu hizo kumi na sita (16) utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.5 ambazo ni mkopo kutoka serikali ya Japani kupitia shirika lake la maendeleo la kimataifa (JICA).

Katika picha kutoka kushoto, Kaimu Mkurugenzi Muhandisi Willson Karumuna, Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Pascal Shayo, Kaimu Mkurunzi Msaidizi Mhandisi Ntonda Kimasa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Mhandisi Muyenjwa Maugo wakifuatila Jambo katika Mafunzo ya wahandisi na wataalam kutoka katika Halmashauri kwenye warsha ya Mafunzo, yalihusu ujenzi wa skimu za umwagiliaji iliyofanyika mkoani Shinyanga.
Katika Picha wahandisi na wataalam wakiwa katika hatua ya mafunzo kwa vitendo katika eneo la Nyida, mara baada ya warsha ya mafunzo iliyohusu ujenzi wa skimu za umwagiliaji iliyofanyika Mkoani Shinyanga.

Hivyo makala TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI
yaani makala yote TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/tume-ya-taifa-ya-umwagiliaji-imetoa.html
0 Response to "TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI"
Post a Comment