Loading...
title : WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO
link : WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO
WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO
*Amwambia Waziri Mkuu kilichofanyika si uungwana, akubali kusamehe yaishe
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
PAMOJA na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kuliomba radhi Bunge kwa kitendo cha Wizara yake kuingia kwenye mgahawa wa Bunge bila kibali na kupima samaki waliopikwa kwa rula, Spika wa Bunge Job Ndugai amasema kitendo hicho ni udhalilishaji.
Juzi Waziri Mpina alitoa maagizo kwa watendaji wa Wizara yake kuingia kwenye Mgahawa wa Bunge na kisha kuingia jikoni kupima samaki ambao tayari walikuwa wamepikwa.Kitendo hicho kilisababisha wabunge kuchachama na kutoa hoja ili kujadili kitendo hicho.Mbunge Peter Serukamba ndio aliyeomba muongozo.
Hivyo leo Mpina akiwa bungeni mjini Dodoma ameomba radhi Bunge pamoja na Spika wa Bunge kwa kitendo hicho.Hata hivyo Spika Ndugai amemueleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji na si sahihi."Tunamshukuru Waziri kutokana na maelezo ambayo ameyatoa lakini niseme tu kwa Waziri Mkuu tumesikitishwa na kilichotokea.
"Sisi si Bunge pekee duniani bali ni sehemu ya mabunge mengine ya jumuiya ya madola.Ikisikika kuna Waziri amefanya kitendo hiki bungeni ni kosa. "Hata kama kuna kosa la jinai ambalo limefanyika ndani ya Bunge ni vema Spika akajulishwa badala ya watu kuingia tu,"amesema Spika Ndugai.
Hivyo makala WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO
yaani makala yote WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/waziri-wa-mifugo-aomba-radhi.html
0 Response to "WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO"
Post a Comment