Loading...

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU

Loading...
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU
link : WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU

soma pia


WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mfugo na Uvuvi atembelea shamba la AKM Glitters Company Ltd lililopo Dar es salaam eneo la Mbopo na Mbezi Beach, ambapo lengo la ziara yake ni kuangalia fursa walizonazo Watanzania katika ufugaji.

Akiwa katika ziara yake katika kampuni hiyo Naibu Waziri ulega ameona kazi mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwemo ya shamba la kuku wazazi, sehemu ya kutotoleshea vifaranga na chakula cha kuku wazazi.Ulega amesema ufugaji wa kuku ni fursa kubwa  ambayo ikiitumia vizuri, mhusika anaweza kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja, na taifa zima kwa ujumla wake.

" Serikali lengo letu ni kuhakikisha nyama ya kuku isiwe kitoweo kwa watu wa juu tu, bali kiwe kwa hali zote kuanzia ngazi ya watu wa kipato cha chini na kati."Tunataka watu wote wajiingize kwenye ufugaji wa kuku, ili tuweze kujitosheleza wenyewe na tutoe ajira nyingi kwa watu ili kuendeleza tasnia hii ya kuku na kuuza kuku kwa bei ya chini kuliko kutegemea kuku kutoka nje,"amesema.

Amefafanua katika bajeti  ya serikali kwa mwaka huu wamependekeza pendekezo ambalo limeletwa Wizara ya Fedha na Mipango, kwamba riba imeondolewa kwa asilimia 5 kutoka kwa wakina mama na vijana."Sasa haitakuwa ni hiari kwa Halmashauri bali ni sheria kuwa Halmashauri zote kadri ya mapato yao ya ndani yanavyopatikana yatakwenda moja kwa moja kwa vijana na akina mama kwa asilima 5 kila mmoja," ameongeza.Amesema Serikali imeona hivyo, ili kusaidia hasa wakina mama walio wengi na kufuta riba hiyo.

Kwa upande wake Mkurugezi Mtendaji wa kampuni hiyo Elizabeth Swai alizungumzia suala la usafirishaji vifaranga ikiwa ni changamoto kuwafikia wakazi wa vijijini ambapo Naibu Waziri alisema, Serikali imejiweka katika mazingira mazuri katika hili kuhakikisha usafirishwaji unawafikia pia watu waliopo vijijini.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia kuku wa wazazi katika shamba la (AKM) lililopo Mbopo jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafanyakazi wa shamba la kuku wazazi,kituo cha kutotolea vifaranga mbopo jijini Dar as Salaam.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shamba hilo.



Hivyo makala WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU

yaani makala yote WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/wizara-ya-mifugo-na-uvuvi-yazungumzia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZUNGUMZIA MIKAKATI YA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA UFUGAJI KUKU"

Post a Comment

Loading...