Loading...
title : ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA
link : ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA
ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 23.6.2018
Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) imewakumbusha Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za Chakula kutoka nje kuhakikisha wanafuata miongozo, sheria na kanuni za usafirishaji ili kuhakikisha bidhaa zao zinafika nchini zikiwa salama kwa matumizi ya wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti wa Chakula na Dawa Dkt. Khamis Ali Omar alisema hayo katika Jaa la Kibele kwenye zoezi la kuteketeza maziwa yaliyoharibika kwa kusafirishwa kwenye kontena moja na mizigo mengine ikiwemo gari kutoka Dubai.
Alisema baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka kutokana na msukosuka wa meli baharini na kuharibu maboksi mengine yaliyopelekea maziwa yote yakose sifa ya matumizi ya binadamu.Aliwashauri wafanyabiashara kuheshimu chakula na kukiepusha na viashiria vyote hatari wakati wa kuvisafirisha na kwenye maghala ili kuwaepusha wananchi na athari zinazotokana na chakula kibovu .
Maziwa hayo yenye uzito wa tani 20 yaliingizwa na mfanyabiashara Essak Suleiman wa Darajani tarehe 6 mwezi huu yakiwa yameshaharibika na kuamua kuyazuia yasiingie sokoni.Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa athari zitokanazo na chakula wa ZFDA Asha Suleiman amewashauri wananchi wanapopewa sadaka ya chakula kuwa waangalifu kwani wamegundua baadhi ya wafanyabiashara hutoa sadaka zilizokwisha haribika baada ya kukosa soko.
Aidha amewashauri wananchi wanapokuwa na shaka ya chakula na kuhisi kinadalili ya kuharibika kutoa taarifa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodi ili kwenda kukiangalia na kupata uhakika wake kabala ya kuanza kukitumia.Wakati huo Mfanyabiashara Essak Suleiman alieingiza maziwa hayo alisema sababu iliyopelekea mzigo huo kuharibika ni upakiaji mbaya uliofanywa na wenye meli, joto kali na kuchelewa kuondoka meli Dubai kuja Zanzibar.
WAFANYAKAZI wa ZFDA wakiteremsha Maziwa yalioharibika kwenye gari kwa ajili ya kuyaangamiza katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
KAIMU Mkurugenzi ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungumzia zoezi la Uteketazaji wa Maziwa tani 20 yalioharibika katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
GARI aina ya Katapila likisaga maziwa yalioharibika na yasiyofaa kwa matumizi ya Binaadamu katika zoezi lililofanyika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Abdalla Omar Maelezo Zanzibar
Hivyo makala ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA
yaani makala yote ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/zfda-wateketeza-tani-20-za-maziwa.html
0 Response to "ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA"
Post a Comment