Loading...

MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA

Loading...
MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA
link : MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA

soma pia


MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza mifumo ya utoaji huduma Serikali kwa njia ya mitandao isitumike kukwamisha shughuli za Serikali au mipango ya utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema watakaobainika kuhujumu mifumo hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu na amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitawavumilia watumishi wasio waadilifu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 23, 2018) mara baada ya kuzindua mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma.Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 iliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU) ni “Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo Endelevu”.

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watumishi wa Umma wote nchini, wananchi, Sekta Binafsi, Sekta ya Umma, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa na Wadau mbalimbali, kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa.“Hii ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika (AU) na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ambayo yamehimizwa na Kaulimbiu ya mwaka huu,”.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza Watendaji Wakuu wa Taasisi zinazosimamia mifumo hiyo pamoja na maafisa waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi kupitia mifumo hiyo, wahakikisha wanailinda na kuitumia vema ili iweze kuwa na tija na manufaa yaliyokusudiwa.

Mifumo hiyo aliyoizundua inahusu utoaji Huduma Serikalini ambayo ni Mfumo wa Usajili wa Vizazi na Vifo, Mfumo wa Taarifa za Kitabibu, Mfumo wa Taarifa za Ununuzi, Mfumo wa Kumbukumbu za Kielektroniki na Mfumo wa Ofisi Mtandao. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kwenye uzinduzi wa mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Katibu Muhtasi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Kholuu Ramadhan, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Johari Swalehe kwa niaba ya mwanae Seif Ramadhan, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Cuthbert Simalenga, wakati akikagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Shukran George kwa niaba ya mwanae Magreth Msomba, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.



Hivyo makala MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA

yaani makala yote MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mitandao-isitumike-kukwamisha-shughuli.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...