Loading...
title : ATCL YADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA SHERIA YA MANUNUZI-NAIBU GAVANA BANK KUU.
link : ATCL YADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA SHERIA YA MANUNUZI-NAIBU GAVANA BANK KUU.
ATCL YADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA SHERIA YA MANUNUZI-NAIBU GAVANA BANK KUU.

Pia imeelezwa, kamati ya wataalam ya Uchunguzi ya Deni la Taifa (TDMC), ilibaini ATCL iliwasilisha maombi ya dhamana kwa Waziri wa Fedha (kwa sasa Wizara ya Fedha na Mipango) kwa kukiuka taratibu za sheria za manunuzi.
Kagandabila ambaye ni shahidi wa upande wa jamuhuri katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 71, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL David Mattaka na wenzake wawili amedai hayo leo Julai 30.2018 wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya washtakiwa hao.
Kabla ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo, Mattaka na washtakiwa wenzie, vigogo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu, Dk. Ramadhan Mlinga na Mwanasheria Bertha Soka. Walisomewa Maelezo ya awali.
Akiongozwa na wakili wa Serikali, Vitalis Peter kutoka Takukuru mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwinzile shahidi huyo alidai ATCL iliwasilisha ombi la kutaka kupata dhamana ikiwa imeisha kiuka sheria yenyewe ya mikopo, dhamana na misaada.Amedai Januari 2008 akiwa Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera na deni la Taifa, ATCL iliwasilisha maombi ya dhamana Wizara ya Fedha kupitia Wizara ya Miundombinu.
Alidai kuwa Januari 11, 2008 walikaa kikao cha TDMC na kubaini kwamba ATCL ilishasaini mkataba wa kukodi ndege bila dhamana ya serikali na kukiuka sheria mbali mbali ikiwemo hawakufuata sheria ya manunuzi ya umma.Pia amedai, maombi ya TTCL hayakuwa yameambatanishwa na maamuzi ya bodi ya ATCL na pia hayakuwa yameambatanishwa na business planing kuweza kusapoti ombi lao hilo.
Amedai kuwa baada ya kubaini hayo, waliwaagiza ATCL kurekebisha kasoro na kuwataka kuonyesha idhini ya bodi kama ilikubakubaliana na ukodishwaji wa ndege hiyo na pia ATCL walitakiwa kuwasiliana na PPRA ili waweze kuonyesha njia waliyotumia kupata ndege hiyo.Hata hivyo, pamoja na yote hayo Waziri wa fedha aliidhinisha kutolewa kwa dhamana hiyo kwa ATCL pamoja na kwamba walikiuka utaratibu kwa kuingia mkataba huo.
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa mkataba ulisainiwa Oktoba 9, 2007 na Mattaka alisaini kwa niaba ya ATCL na Andrew Wettern kwa niaba ya Wallis Trading Inc na kuisababishia Serikali hasara.
Hivyo makala ATCL YADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA SHERIA YA MANUNUZI-NAIBU GAVANA BANK KUU.
yaani makala yote ATCL YADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA SHERIA YA MANUNUZI-NAIBU GAVANA BANK KUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ATCL YADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA SHERIA YA MANUNUZI-NAIBU GAVANA BANK KUU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/atcl-yadaiwa-kukiuka-taratibu-za-sheria.html
0 Response to "ATCL YADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA SHERIA YA MANUNUZI-NAIBU GAVANA BANK KUU."
Post a Comment