Loading...
title : CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA
link : CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA
CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA
*Ni ya mwamvuli unaotumia mionzi ya jua kutengeneza umeme, kuanza kutumika Karagwe
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
CHAMA cha Kukuza Uhusiano kati za Tanzania na China umefanikisha kupatika kwa msaada wa miavuli 100 inayotumia nguvu ya jua kuzalisha umeme ambayo imekabidhiwa kwa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Miavuli hiyo ambayo ni teknolojia mpya iliyozinduliwa China inakwenda kuanza kutumika wilayani humo kwenye baadhi ya shule, zahanati na kituo cha afya kwa lengo la kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana kwa ustawi wa maendeleo ya nchi yetu.
Msaada huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Maendeleo ambayo ipo chini ya Chama cha Kikomunisti cha China(CPC).
Hivyo Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa CPC Song Tao ndio aliyokabidhi msaada huo ambapo amesema wanatambua urafiki , udugu na ujamaa wa nchi hizo mbili na hivyo wanatambua umuhimu wa kuendelea kuisaidia Tanzania.
Akizungumzia msaada huo Katibu Mkuu wa Chama cha Kukuza Uhusiano wa Tanzania na China Joseph Kahama amesema msaada huo umetokana na jitihadaza chama chao katika kuhakikisha uhusiano wa nchi hizo mbili unaendelea.
Amefafanua kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kuzinduliwa kwa teknolojia hiyo ambayo kwa hapa nchini itakwenda kuanza kutumika wilayani Karagwe.
Pia amesema kwenye vituo vya afya na zahanati msaada huo unakwenda kusaidia kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya na kueleza miavuli hiyo inaweza kutumika katika vifaa mbalimbali vinavyotumia umeme.
"China imeamua kuitumia Tanzania kuzindua teknolojia hiyo ambayo haiko mahali kokote duniani .Tumepewa miavuli 100 na mingine itaingia nchini Oktoba mwaka huu .
Alipoulizwa kuhusu thamani ya msaada huo amejibu kuwa hawezi kuifahamu ila anachojia teknolojia mpya nayo ina gharama zake.
Awali Mwenyekiti wa Chama cha Kukuza Uhusiano wa Tanzania na China Dk.Salim Ahmed Salim ameipongeza nchi ya China kwa msaada huo na ni uthibitisha unaodhihirisha urafiki wao wa muda mrefu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA
yaani makala yote CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/china-yaitumia-tanzania-kuzindua.html
0 Response to "CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA"
Post a Comment