Loading...
title : DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI
link : DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI
DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI
Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Idd Hassan Kimanta jana Julai,11/2018 amezindua kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi na kutengeneza bidhaa za ngozi kiwanda hicho kipo katika kijiji cha Mswakini na kutoa vyeti kwa wanakikundi waliofuzu mafunzo.
kiwanda hicho ni matokeo ya kikundi cha akinamama 22 ambao mwezi Agosti 2017 walijiunga pamoja na kupata ufadhili kutoka shirikikala OIKOS kwa lengo kujijenga kiuchumi kupitia Ngozi na kuunga mkono Juhudi za Serikaliya kuelekea Tanzania ya Viwanda.
Katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya amewapongeza akinamama hao kwa uamuzi wao huo na kuwaahidi kuwa ,kupitia Halmashauri ya Wilaya Monduli atahakikisha wanapata Mkopo ili kuongeza mtaji.
Pia amelishukuru Shirika la Misaada la Marekani-USAID kwa kulipatia fedha shirika la OIKOS ambalo ndilo lililosimamia mchakato wote kupitia Mradi wa Ikolojia Hatarini Kaskazini mwa Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta (pichani kati) akitazama baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi kilichopo katika kijiji cha Mswakini,wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Idd Hassan Kimanta akitoa vyeti kwa baadhi ya Wanakikundi waliofuzu mafunzo.
Baadhi ya Bidhaa za ngozi zikiwa tayari kwa kuuzwa
Hivyo makala DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI
yaani makala yote DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/dc-monduli-azindua-kiwanda-kidogo-cha.html
0 Response to "DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI"
Post a Comment