Loading...
title : GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA
link : GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA
GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima hii leo amefanya ziara ya kikazi katika Gereza Kuu la Isanga lililopo Jijini Dodoma na kuutaka uongozi wa Gereza hilo kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa kupanda miti zaidi na kuacha matumizi yasiyoendelevu ya mkaa na kuni kama nishati ya kupikia.
Akizungumza na Uongozi wa Gereza hilo Mhe. Sima amewataka kutumia majiko banifu ili kupunguza kasi ya ukataji miti kwa matumizi ya kupikia. “Natoa wito kwenu kuanza kutumia teknolojia mbadala ya kuni na mkaa kama nishati ya kupikia na kuwaagiza kuona namna bora ya kutumia gesi ili kunusuru misitu yetu”
Pia, Waziri Sima ameagiza uongozi wa gereza hilo kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kuotesha miti inayostahimili ukame kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na shamba darasa kwa watu kujifunza kilimo hicho cha miti na kutoa ushauri wa kitaalamu.
Akitoa taarifa ya Gereza hilo Naibu Kamishna wa Magereza Julius Mayenga Sang’udi amesema kuwa kwa siku gereza hilo hutumia wastani wa kuni mita za ujazo 8-10 kwa matumizi ya kupikia, kuni ambazo hutolewa katika kambi ya Mayamaya, Taasisi za Serikali na ujenzi binafsi.Kufuatia maelekezo ya Naibu Waziri, Kamishna Sang’udi amesema kuwa mpango uliopo sasa ni kugeuza changamoto kuwa fursa ikiwa ni pamoja na kuhuisha wazo la kujenga mfumo wa matumizi ya gesi na ‘biogas’ kama nishati ya kupikia.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akisalimiana na Uongozi wa juu katika Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma. Ziara ya Naibu Waziri katika gereza hilo imelenga kuhimiza viongozi hao kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Dodoma ya Kijani’
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Ranchi ya Kongwa mara baada ya kutembelea ranchi hiyo mapema leo. Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri amemuagiza Meneja huyo kuwa na mpango kabambe wa upandaji miti katika eneo hilo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Ranchi ya Kongwa mara baada ya kutembelea ranchi hiyo mapema leo. Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri amemuagiza Meneja huyo kuwa na mpango kabambe wa upandaji miti katika eneo hilo.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa Bw. Euzebius Mutayabarwa akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa namna ya shughuli za hifadhi ya mazingira zinavyotekelezwa katika eneo lake. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine na viongozi wa Wilaya ya Kongwa.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa Bw. Euzebius Mutayabarwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na ujumbe wake mara baada ya kutembelea ranchi hiyo leo iliyopo Wilayani Kongwa Jijini Dodoma.
Hivyo makala GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA
yaani makala yote GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/gereza-kuu-la-isanga-laagizwa-kutumia.html
0 Response to "GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA"
Post a Comment