Loading...
title : LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA.
link : LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA.
LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA.
Katibu wa HKT Siasa na uhusiano wa kimataifa Cde Ngemela Lubinga ameanza ziara yake ya kampeni katika Kata ya Nyamichige wilaya ya Ruangwa na jimbo LA Ruangwa.
Katika mkutano huo cde Ngemela Lubinga aliwasisitiza wananchi wa kata ya Nyamichige wamchague diwani Ndg Mikidadi Ibadi Matauna almaarufu Mbute ambaye alihama Chama cha Chadema na kujiunga na CCM kutokana na Chama hivyo kushindwa kumpa ushirikiano wa kutosha kama diwani na kumtenga mara kwa mara anapozisifia jitihada za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Cde Lubinga amewaomba wananchi hao wamchague diwani huyo ili kuweza kukamilisha safu ya uongozi katika jimbo hilo kwani kwa kufanya hivyo hawataipa heshima CCM peke yake kama Chama kilichowaletea maendeleo katika wilaya ya Ruangwa lakini pia itakuwa ni heshima kubwa kwa mbunge wa jimbo hilo ambaye Rais Dr John Pombe Magufuli alimpa heshima ya kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano.
Aidha cde Lubinga aliendelea kusisitiza kuwa maendeleo yanayoendelea kupatikana katika jimbo la Ruangwa ni juhudi kubwa za mbunge wa jimbo hilo Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa,Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Cde Lubinga amewasisitiza wananchi katika kata ya Nyamichige kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma pamoja na kuhakikisha vijana wao wanawapeleka shuleni na pia kuhakikisha wanatokomeza mimba za mapema kwa watoto wa kike ili waweze kuwa viongozi wa kesho.
Mwisho cde Lubinga alichukua wasaa wake kumpongeza mbunge wa jimbo la Ruangwa Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa kwa kuwa anaweza kuwa ni Waziri Mkuu wa kwanza kuweza kufanya ziara katika kata zote 22 za jimbo la Ruangwa na pia vijiji 88 kati ya vijiji 90 vilivyopo katika jimbo la Ruangwa kwani kwa kufanya hivyo ameonyesha mfano kama kiongozi wa kitaifa.
Hivyo makala LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA.
yaani makala yote LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/lubinga-aunguruma-katika-kata-ya.html
0 Response to "LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA."
Post a Comment