Loading...
title : GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN)
link : GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN)
GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN)
Na Luteni Selemani Semunyu.
Klabu ya Gofu ya jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo imetamba kuendeleza wimbi la ushindi katika Mchezo huo kupitia timu yake yenye wachezaji 30 inayotarajia kusafiri kuelekea Mufindi mkoani Iringa kushiriki mashindano ya wazi ya Mufindi yanayotarajiwa kufanyika Julai 27 hadi Julai 29 katika Viwanja vya Klabu hiyo
Akizungumza na Waandishi wa habari mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu alisema Timu inatarjiwa kuondoka Julai 26 kuelekea Mufindi ambapo mbali na wachezaji wa Ridhaa wapo wachezaji wa kulipwa Sita ambao nao wamejipanga kufanya vyema..
“ Tunawachezaji wengi nyota na chipukizi wengine wapo kwenye majukumu ya kazi lakini wengine wako katika kuwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa kwa kuwa tuna vipaji vya kutosha tutapeleka Timu nzuri na kupata Ushindi” Alisema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.
Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo aliwataja Wachezaji wa Kulipwa wa Klabu ya Lugalo watakaowakilisha katika Mashindano hayo kuwa ni David Helela, Abdalah Yusuph, Geofrey Leverian na Brison Nyenza , Iddi Mzaki aliyechukua nafasi ya tatu katika mashindano ya wazi ya Lugalo na Athumani Chiundu.
Mshindi wa kwanza wanawake kutoka klabu ya Gofu ya Lugalo Habiba Likuli akipiga mpira wakati wa mashindano ya wazi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam anayemuangalia ni Amanda Mlula wa klabu hiyo( Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Baadhi ya Wachezaji wa klbu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakiwa katika mazaoezi katika uwanja wa Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Hivyo makala GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN)
yaani makala yote GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/gofu-lugalo-yatamba-kuibuka-na-ushindi.html
0 Response to "GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN)"
Post a Comment