Loading...
title : Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata
link : Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata bali waendelee kujitoa katika kuokoa maisha ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima alipokuwa akizungumza na wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Gwajima alisema hivi sasa Taasisi hiyo imekuwa tegemeo kubwa kwa wagonjwa wa moyo kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati hivyo basi ufanyaji kazi kwa ufanisi utasaidia wananchi wengi kuendelea kupata huduma za matibabu ya moyo hapa nchini.
“Jamii ya Tanzania inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na JKCI, nawasihi wafanyakazi msikubali changamoto yoyote ile inayowakabili ikaitoa Taasisi hii katika mstari wa mafanikio mliyoyapata”. Habari zaidi SOMA HAPA
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi tuzo ya utendaji kazi bora wa Idara ya Magonjwa ya Moyo ambayo ni moja ya Kurugenzi tano za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo ambaye pia ni daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpongeza Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Ghati Chacha kwa ajili ya utendaji kazi mzuri wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha walioufanya kwa kipindi cha miezi mitatu wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza washindi iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima.
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo ya utendaji kazi bora wa Kitengo cha manunuzi David Kakoti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika hafla fupi ya kuzipongeza Idara na Vitengo vilivyofanya kazi vizuri kwa kipindi cha miezi mitatu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada wakati wa kikao na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika kivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Tiba Tanzania Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo daktari bingwa wa upasuaji wa Moyo Dkt. Evarist Nyawawa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutokana utendaji kazi bora wa kitengo cha upasuaji wa Moyo wakati wa kikao na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.Picha na Brighton James -JKCI.
Hivyo makala Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata
yaani makala yote Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wafanyakazi-wa-taasisi-ya-moyo-jakaya.html
0 Response to "Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata"
Post a Comment