Loading...

KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5

Loading...
KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5
link : KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5

soma pia


KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) wamefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 15.5 kwa mwaka mzima wa fedha 2017/2018 kuanzia julai 2017 hadi Juni 30 2018 ukilinganisha na shilingi trilioni 14.4 zilizokusanywa mwaka wa fedha 2016/2017.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo ameeleza kuwa kiasi kilichokusanywa ni sawa na asilimia 7.5 kiukuaji na kwa mwezi Juni pekee TRA imekusanya shilingi trilioni 1.5 ukilinganisha na trilioni 1.4 zilizokusanywa mwezi Juni mwaka 2017.

Aidha ameeleza kuwa sababu za kuongezeka kwa makusanyo hayo ni pamoja na uwepo wa elimu ya kodi inayowasaidia walipakodi na wananchi kwa ujumla kutambua umuhimu wa kulipa kodi, kuwa karibu na walipa kodi sambamba na kutatua changamoto zao za kikodi, kuongezeka kwa walipa kodi wapya  kupitia kampeni ya kuwasajili kwa kuwafuata waliko na kurahisisha ulipaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki.

Pia ameeleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha TRA imedhamiria kutekeleza kwa vitendo kampeni kabambe ya msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma na wanataraji kuongeza urahisi wa kulipa madeni ambayo yalikuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wengi kulipa na hata kuendelea na biashara.

Kayombo amesema kuwa wamedhamiria kuongeza kasi ya usajili wa walipakodi wapya na wanaendelea na kasi ya utambuzi na usajili wa wafanyabiashara wadogo ili kila mtu anayestahili kulipa kodi asajiliwe na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

Kwa niaba ya mamlaka hiyo amewashukuru na kuwapongeza walipa kodi wote ambao mchango wao umeiwezesha serikali kupata mapato ambayo yatasaidia shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu,  upatikanaji wa elimu, afya na mambo mengine mengi yenye manufaa kwa watanzania wote.

Kayombo ametoa wito kwa walipa kodi wote kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kujenga utamaduni wa kutoa na kudai risiti za kielektroniki na kutolea risiti (EFDs.)
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa taarifa ya makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.


Hivyo makala KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5

yaani makala yote KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/kusanyo-la-kodi-mwaka-wa-fedha-20172018.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5"

Post a Comment

Loading...